Serikali yawaagiza Viongozi kutokuwa na Muingiliano wa majukumu

Na Hosseah Nteghenjwa

Serikali yawaagiza Viongozi kutokuwa na muingiliano wa majukumu

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote nchini kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi ili kutimiza matarajio ya watanzania ambao wanategemea kupata chachu ya mabadiliko katika utendaji kazi wa Serikali ya awamu ya Tano.

Mhe.Jafo ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mikoa ya Dar es Salaam, Shinyanga, Mbeya, Songwe, Rukwa, Ruvuma, Iringa na Njombe yanayoendeshwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa ushirikiano na Taasisi ya Uongozi.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo Mhe.Jafo amewataka viongozi hao kutumikia Wananchi kwa kuzingatia Taratibu, Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma huku wakizingatia mipaka yao ya Utawala, kuboresha mahusiano katika maeneo ya kazi na kuhakikisha hakuna muingiliano wa majukumu baina ya viongozi wa Wilaya na Halmashauri.

“Nafahamu baadhi viongozi mlitokea katika sekta binafsi na humkuwa mnafahamu vizuri utendaji kazi wa shughuli za Serikali hata hivyo mmefanikiwa kwa kipindi chote kutenda kwa kadiri ya maelekezo ya Serikali,vipaumbele na miongozo mbalimbali iliyotolewa pia mmejitahidi kutoa huduma bora ukiachilia mbali mapungufu madogo madogo ambayo tumeyabaini na kuyashuhudia katika baadhi ya maeneo” alisema Jafo.

Aliongeza kuwa matumaini ya Serikali baada ya mafunzo hayo Viongozi hao watakuwa na uelewa wa pamoja kwani lengo ni kuitumikia Serikali na kutimiza azma ya Serikali ya awamu ya tano. “kupitia mafunzo haya ni imani yangu kuwa wote sasa tutakuwa na uelewa wa pamoja wa kufanya kazi Kimkakati ili kuwaletea wananchi maendeleo huku mkifahamu vyema Muundo wa Serikali na namna inavyofanya kazi kwa kuzingatia mipaka na mgawanyo wa majukumu, Itifaki, utunzaji wa Siri za Serikali na maadili ya viongozi wa Umma”

Aidha, aliwataka viongozi hao kuendelea kusimamia nidhamu ya watumishi, kuendeleza mapambano dhidi ya Dawa la kulevya, kulinda amani na utulivu katika maeneo yao huku wakisimamia kwa makini mapato na matumizi ya Fedha za Serikali na kusisitiza matumizi ya mifumo ya Kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali.

Kwa upande wake Naibu Katibu (Afya) OR - TAMISEMI Dkt. Zainabu Chaula amesema kitu cha msingi kwa watendaji ni umoja ambao utatuleta ushindi na muongozo wa utendaji kwenye Ilani ya Chama Tawala.

p align="justify"> Awali katika taarifa ya utangulizi kabla ya hotuba, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja alisema mafunzo haya yanatolewa na wataalamu walioboea katika masuala ya uongozi ambayo yatawajengea uwezo wa kufanya maamuzi ya kimkakati yanayozingatia maslai ya Taifa.

p align="justify"> Awamu ya kwanza ya mafunzo haya ya Uongozi yalifanyika Mwezi Mei, 2017 na yalifunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na awamu ya mwisho inatarajiwa kufanyika kabla ya mwezi Disemba, 2017.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.