Serikali yawataka Wataalam kufanya kazi kwa bidii, weledi na ubunifu

Na. Fred J. Kibano

Serikali yawataka Wataalam kufanya kazi kwa bidii weledi na ubunifu

Serikali imewataka Makatibu Tawala Wasaidizi, Maafisa Mipango na Maendeleo ya Jamii katika Mikoa na Halmashauri kufanya kazi kwa weledi, ubunifu na kwa kujituma ili kuchochea maendeleo tarajiwa kama inavyoelekeza katika Ilani ya Chama Tawala lengo likiwa kutoa huduma bora na kuleta maendelo kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu (Afya) Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt Zainab Chaula wakati wa mafunzo ya siku moja kwa Makatibu Tawala Wasaidizi, Maafisa Mipango na Maendeleo ya Jamii ngazi ya Mikoa na Halmashauri kuhusu Tuzo za Waziri OR TAMISEMI kwa mwaka 2018 kwa vijiji vitakavyofanya vizuri katika kujiletea maendeleo kwa ushiriki wao na nguvu zao katika sekta kama barabara, utawala bora, majengo ya shule na mengineyo inayojulikana kama Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo Iliyoboreshwa.

“Ndugu zangu, kuna watu wapo wana vipaji lakini hawataki kufanya mpaka waambiwe, tumeletwa hapa kama Viongozi tupate mafunzo na tukayafanyie kazi. Nategeme kwenye Tuzo, wote mtapata tuzo”

Dokta chaula amewataka Watendaji hao kushirikisha vijiji na wananchi katika mipango yao ili kujiletea maendeleo na kwamba Tuzo ya Waziri kwa kijiji bora iwe chachu ya uwajibikaji na ushirikishwaji wakati wote wa mchakato wa kutafuta kijiji bora. Amewataka kufanya kazi kama timu ili kufikia malengo ya Ilani ya Chama Tawala, “katika utumishi wetu wa Umma, tujiulize tumefanya nini?, lazima tufanye kama timu, zingatieni kutenda kazi kama inavyotaka Ilani ya Chama cha Mapinduzi”, ambayo inawataka watumishi wenye sifa tatu za weledi, uadilifu na uwajibikaji lakini pia kuleta maendeleo ya wananchi na kudumisha amani, upendo, umoja na mshikamano.

Dokta Chaula amewataka pia kuwa karibu na wananchi ili kujua matatizo yao na kuyapatia ufumbuzi hali wakiwa pamoja kama inavyosisitiza Serikali ya awamu ya tano. “Siku zote tuambiane ukweli juu ya utendaji mzuri, ni lazima wote tuambiane ukweli, tutembee pamoja na tufanye kama Serikali ya awamu ya tano inavyotaka”, kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kuleta maendeleo na kutoa huduma bora kwa jamii yote ya Watanzania ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa sahihi kwa wakati.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Serikali za Mitaa OR TAMISEMI Jenister Kihaga amesema kwamba mafunzo hayo yatasaidia kuleta chachu kwa wananchi na washiriki wote kwa kupata hamasa ya kufanya kazi kwa weledi ili kuleta maendeleo vijijini na kwa Watanzania wote lakini pia Halmashauri kuwatumia vema Maafisa Maendeleo ya Jamii. Aidha, amesisitiza kuwa Serikali Kupitia OR TAMISEMI imejiwekea malengo katika kukamilisha miradi viporo kama vile maboma ya shule na zahanati katika Halmashauri zote ili kuepukana na adha ya kutokamilika miradi mingi inayoibuliwa na wananchi kila mwaka na kuishia njiani bila kuwa na tija yoyote. “Maafisa Maendeleo ya Jamii hawatumiki ipasavyo, tunataka mradi wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O and OD) iliyoboreshwa ikatumike kama chachu ili kuleta maendeleo, ikiwa ni pamoja na kukamilisha miradi viporo”

Baadhi ya vijiji vinavyotarajiwa kushiriki Tuzo ya Waziri ni pamoja na maseyu, matema, nakafulu, libenanga na mang’ula B vyote kutoka mkoani Morogoro, vingine ni kutoka wilaya za Bagamoyo,Kisarawe,Chalinze,Morogoro,Ulanga,Kilombero,Kondoa,Siha,Same na Hai. Tuzo ya Waziri ambayo itaanza kutolewa mwaka huu kwa kijiji bora ni mpya na inalenga katika kukuza ushirikiano, kuleta ushindani wa kimaendeleo na kupunguza gharama za utekelezaji wa miradi kwa wananchi kushiriki moja kwa moja katika miradi ambayo wataiibua wao wenyewe bila kuingiliwa na Mamlaka yoyote.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.