Serikali yawaagiza watumishi kuleta mabadiliko katika utendaji kazi

Angela Msimbira


Serikali yawaagiza watumishi kuleta mabadiliko katika utendaji kaz

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe amewaagiza Waratibu wa mikoa, Mameneja na Wahasibu wa Halmashauri zote nchini kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma na kuleta mabadiliko katika jamii.

Akifungua kikao kazi cha utekekezaji wa majukumu ya Wakala wa barabara za Vijijini na Mijini kwa Waratibu wa Mikoa, Mameneja na Wahasibu wa Halmashauri. Katibu Mkuu (OR-TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe amewataka watumishi wa serikali kuzingatia weledi kwa kutumia taaluma walizonazo katika kutoa huduma sahihi kwa wananchi.

“Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) ni taasisi mpya, inahitaji kuwa mfano kwa jamii kwa kutekeleza majukumu kwa jamii bila kujihusisha na rushwa kutoka kwa Wakandarasi jambo ambalo limekuwa ni changamoto kubwa na kurudisha nyuma maendeleo katika jamii”.Amesema Mhandisi Iyombe. Amesema ufike wakati ambapo watumishi wanajituma katika kutekeleza majukumu waliojiwekea ili kuonyesha mabadiliko kwa wananchi na kuiwezesha Serikali kutimiza malengo waliyojiwekea katika kutoa huduma bora kwa maendeleo ya Taifa.

Amesema Serikali imeandaa mazingira mazuri ya kufanyia kazi ili kuwawezesha kutenda kazi kwa ufanisi hivyo ni wajibu wa kila mtumishi kufanya kazi kwa uadilifu, weledi na uaminifu mkubwa kwani Serikali haitasita kumchukulia hatua mtumishi yeyote ambaye atakiuka kanuni na sheria zilizowekwa na Serikali.

“Acheni utaratibu wa kuchukua rushwa kwa Wakandarasi, suala hili linarudisha nyuma maendeleo ya nchi na kutoa sifa mbaya kwa wananchi, ni wakati sasa wa kubadilisha mienendo yenu katika kutoa huduma kwa uaminifu kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma”.Amesema Mhandisi Iyombe.

Mhandisi Iyombe amesema kuwa wananchi wana imani kubwa na Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini katika kuwaletea maendeleo, umefika wakati wa kubadilika kwa kujiwekea mikakati na kuweka vipaumbele ili kutimiza malengo ya Serikali, hivyo tuhakikishe wanafanya kazi kwa kufuata misingi na maelekezo kutoka Serikalini.

Aidha amesema mategemeo ya Serikali ni kuwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) itabadilisha maendeleo ya wananchi kwa kuleta maendeleo kwa kuwa wananchi wanategemea barabara kwa ajili ya shughuli za kiuchumi, kisiasa na kijamii hivyo wafanyekazi walizotumwa na Serikali ili kutimiza lengo la Serikali la kwenda na viwanda ili kuleta maendeleo katika nchi.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.