Wadau wa Elimu : Wekezeni kwenye maeneo yenye uhitaji

Na. Angela Msimbira

Naibu Katibu Mkuu Elimu atoa wito kuwekeza kwenye maeneo yenye uhitaji maalum
--------------------------------------------------

Naibu Katibu Mkuu , Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa upande wa elimu Bw. Tixon Nzunda ametoa wito kwa wadau wa sekta ya elimu nchini kuwekeza kwenye maeneo yenye uhitaji ili kuongeza tija na kuleta maendeleo kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Ameyasema hayo kwenye Kikao cha pamoja kati shirika la Marekani la maendeleo ya Kimataifa (USAID) kupitia mradi wa Tusome Pamoja na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kilichofanyika katika ukumbi wa TAMISEMI Mjini Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Elimu Bw. Nzunda amesema Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imejiwekea mkakati wa kuwahudumia wananchi wa ngazi za nchini ili kuwaletea maendeleo katika jamii.

“TAMESEMI kwa sasa imejikita kutoa huduma stahiki kwa jamii yenye uhitaji ili kuleta chachu ya maendeleo katika maeneo ambayo yamesaulika katika miradi mbalimbali inayotolewa na Serikali lengo likiwa ni kuongeza ufanisi na kufikia walengwa wa mahitajji hayo.” Amesema Bw. Nzunda

Amesema wafadhili wajikite katika kuwekeza katika sekta ya afya,elimu ili kuweza kuwasaidia wananchi wenye mahitaji muhimu na kuacha kufanya kazi kwa mazoea ili kuleta matokeo nyanya kwa Serikali.

“Kumekuwepo na Miradi mingi ambayo imekuwa ikitekelezwa na wafadhili mbalimbali nchini lakini mingi inashindwa kuendelea kutokana na miradi hiyo kutofanya tathmini ya kina ya mahitaji halisi ya wananchi”Amesema Bw. Nzunda.

Amesema kuwa ifike wakati kila mtumishi atimize majukumu yake kwa kufanya kazi kwa weledi , kuwatumikia wananchi na kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofadhiliwa na mashirika mbalimbali hapa nchini, miradi hiyo iwanufaishe wananchi wa chini ambao ndio wenye uhitaji mkubwa na kufikia lengo la kuleta maendeleo kwa jamii.

Bw. Tixon Zunda amesema Serikali haitasita kuwachukulia hatua watumishi ambao ni wasimamizi wa Miradi ya serikali ambao hawatimizi majukumu yao kikamilifu, hivyo wafanye kazi kwa manufaa ya nchi.

Amesema Miradi inayotekelezwa na kufadhiliwa na Serikali ya Merekani ikiwepo sekta ya Elimu na inatekelezwa Kupitia Shirika la Merekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) Kupitia mradi wa Tusome Pamoja

Mradi wa Tusome Pamoja unasaidia kuboresha Elimu ya Msingi kwa kutumia zana mpya za kufundishia na kujifunzia, Mafunzo kwa waalimu na wasimamizi wa shule na kuongeza ushiriki wa wazazi na jamii katika uendeshaji wa shule na utoaji wa Elimu.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.