Serikali yaagiza Halmashauri kutoa mafunzo kwa wakulima kuboresha uzalishaji wa mazao

Serikali yaagiza Halmashauri kutoa mafunzo kwa wakulima kuboresha uzalishaji wa mazao
--------------------------------------------------

Naibu Waziri OR TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo ameziagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa kuweka utaratibu wa kuwaelimisha wakulima kuwa na mifugo michache na bora kuliko kuwa na utitiri wa mifugo isiyo na tija ambayo pia hupelekea migogoro baina yao na wakulima.

Mhe.Jafo ametoa kauli hiyo wakati akifunga maonyesho ya kilimo Nane nane kwa Kanda ya Kati mjini Dodoma kwa kusema elimu kwa wafugaji, wakulima na wavuvi liwe endelevu ili kuzalisha kwa tija hasa malighafi bora za viwanda kama ilivyo katika kauli mbiu zalisha kwa tija mazao ya bidhaa za kilimo, mifugo na uvuvi ili kufika uchumi wa kati.

Aidha, amewataka Viongozi wa Mikoa na Halmashauri kutenga maeneo ya viwanda ili yenye barabara, maji, miundo mbinu yote ili wawekezaji wapate maeneo rafiki yatakayowawezesha kufanya kazi ya uzalishaji kwa urahisi zaidi.

Amewataka wananchi wa Dodoma na Singida kutumia fursa za kijiografia zilizopo kama kilimo cha alizeti, karanga na zabibu ili kuchangia malighafi ya mazao haya kwenda katika viwanda yakiwa yanatoka kwenye maeneo yao.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula, Uvuvi na Mifugo Mhe. William Ole Nashe amesema idadi ya washiriki kwa ajili ya kuonesha bidhaa imeongezeka kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo matumizi ya barcode kwa ajili ya kusajili biasharapia yameongezeka. “Tumejipanga kuhakikisha sekta ya kilimo inakua kulingana na mahitaji ya wakulima, wafugaji na wavuvi”

Aidha, Tanzania imepiga hatua katika utafiti wa mazao kwa mfano ndiyo nchi yenye korosho bora Duniani.

Changamoto zinazoikabili sekta hii ni pamoja na mabadiliko ya tabia ya nchi, ukame na mengineyo na ndio maana Wizara ya kilimo imeandaa mwongozo wa kilimo kwa wadau juu ya namna ya kuzalisha mazao kwani tayari umefanyika ugunduzi wa mbegu kumi na moja za mahindi chotara ili kuzalisha chakula. Mpango uliopo ni kuhimiza sekta binafsi kuzalisha mazao kwa kasi Wizara imefuta ushuru wa mazao yapatayo tani moja kusafirisha kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Serikali imeagiza tani 32,000 za mbolea aina ya Urea na tani 33,000 za mbolea ya kupandia aina ya ADD ambazo zitaingia nchini kwa ajili ya kukabiliana na upungufu na kuboresha mazao.

Kauli mbiu kwa mwaka huu inasema, “zalisha kwa tija mazao na bidhaa za kilimo, mifugo na uvuvi ili kufika uchumi wa kati”. Maonyesho haya yamefanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi, Nzuguni Dodoma, Mbeya, Morogoro, Arusha na Mwanza.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.