Serikali yahamasisha matumizi ya Teknolojia ya kilimo kwa Wakulima ili kuleta maendeleo endelevu

Na. Nteghenjwa Hosseah

Serikali yahamasisha matumizi ya Teknolojia ya kilimo kwa Wakulima

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George B. Simbachawene (Mb) amewaagiza Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini sambamba na Maafisa Ugani kujifunza Teknolojia mbalimbali zilizopo kwenye maonyesho ya nane nane Jijini Arusha na kwenda kuwafundisha wananchi ili wawezesha kutekeleza katika maeneo hayo.

Akifungua Maonyesho hayo ya 24 Kanda ya Kaskazini yaliyofanyiika Mkoani Arusha katika viwanja wa Themi – Njiro, amesema anatarajia maonyesho hayo kuwa yataleta mabadiliko kwa wananchi kwa kuwawezesha kulima kwa tija kwa kutumia eneo dogo na kuweza kupata mazao mengi, kufunga kisasa kwa kuwa na mifugo bora na michache lakini yenye faida kubwa pamoja na kuanzisha ufugaji bora wa samaki katika maeneo mengi nchini.

“Kuanzia mwakani tutaanza kufanya tathmini ya namna ambavyo maonyesho haya yamebadilisha maisha ya wakulima wetu katika Halmashauri na sio kila mwaka Halmashauri zinashiriki lakini hamuondoki na kitu kipya wala hamuwasaidii wakulima wa kule vijijini ambao huenda hawapati fursa ya kuja kuona mapinduzi haya katika Kilimo”

Wakati wa Ufunguzi wa Maonyesho hayo Waziri Simbachawene alikagua mabanda mbalimbali ya Kili mo na Mifugo ya Halmashauri za Kanda ya Kaskazini, Sekta binafsi za Kuzalisha Mbegu bora, Pembejeo, Zana za Kilimo viwatilifu pamoja na dawa za Mifugo na kujionea teknolojia bora na za kisasa zinazoweza kumsaidia Mkulima na Mfugaji kuachana na kilimo cha kujitaftia chakula na kuhamia kwenye biashara njia itakayoweza kumuo ngezea kipato na kumwinua kiuchumi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya maonyesho haya Kanda ya Kaskazini amesema maonyesho haya yametoka kwenye Chama cha Wakulima na Wafugaji (TASO) na kuratibiwa na Serikali na wamejitahidi kushirikisha Wadau mbalimbali wenye teknolojia tofauti tofauti ili kuweza kutoa wigo mpana kwa wakulima na wafugaji kujifunza zaidi.

Pia aliongeza kuwa ameunda kamati ambayo itaongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro kuchunguza namna ambavyo TASO walivyokuwa wanafanya kazi, Mali zinazomilikiwa na Taso, Mapato yaliyopatikana wakati wa uratibu wao na namna ambavyo yalitumika na mgawanyo wa kazi zao na kuja na mgawanyo wa kazi zao na kuja na usahuri wa kitaalam juu ya nini kifanyike katika kuboresha zaidi usimamizi wa maonyesho hayo.

Waziri wa Nchi Mhe. Simbachawene amefungua maonyesho haya ikiwa ni ya Pili tangu maadhimisho ya Sherehe hizi yalipoanza na alifungua maonyesho haya Kitaifa katika Viwanja vya Ngongo – nje kidogo ya Manispaa ya Lindi na anatarajiwa kufunga maonyesho haya pia katika viwanja vya John Mwakangale Mkoani Mbeya.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.