Serikali yaagiza Taasisi binafsi kuandaa Miradi ya thamani halisi

Na. Angela Msimbira

Serikali yaagiza Taasisi binafsi kuandaa Miradi ya thamani halisi

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe amezitaka taasisi zisizo za Serikali za Sekta ya Afya nchini kuandaa miradi inayoendana na mahitaji halisi ya wananchi ili kutoa huduma sahihi kwa jamii na kuleta maendeleo kwa Taifa.

Mhandisi Iyombe ametoa wito huo wakati akifungua kikao cha pamoja kati ya Wakuu wa Taasisi zisizo za kiserikali za Sekta ya Afya na Makatibu Wakuu wa OR-TAMISEMI na Wizara ya afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kilichofanyika katika ukumbi wa TAMISEMI, mjini Dodoma.

Mhandisi Iyombe amesema kuwa miradi mingi ambayo imekuwa ikitekelezwa na Wadau mbalimbali wa afya hailengi kutatua matatizo ya wananchi na hakidhi mahitaji halisi ya jamii hivyo ifike wakati wadau wa Afya kuandaa miradi ambayo inaendana na mahitaji stahiki ya wananchi.

“Miradi ya Afya ilenge kuwasaidia wananchi katika ngazi ya nchini, kwani kumekuwa na malalamiko mengi juu ya utoaji wa huduma za afya katika ngazi ya za vijiji, Kata, Wilaya na Mikoa”,Amesema Mhandisi Iyombe.

Aidha, amesema kuwa kuna taasisi nyingi sana zinazojihusisha na afya lakini hakuna matokeo ya kuwasaidia wananchi ndio maana kule kwa wananchi hakuna matokeo hasi ya miradi inayotekelezwa na mashirika mbalimbali yanayojitokeza kutoa misaada kwa Serikali.

“Wafadhili wamekuwa wakitoa fedha nyingi kwa ajili ya kuwekeza katika Miradi mbalimbali ya afya lakini matokeo yamekua hasi kwa jamii kutokana na fedha hizo kutoendana na matumizi halisi katika utekelezaji wa miradi hiyo”, Amesema.

Amesema wananchi wanakosa huduma muhimu katika sekta ya afya, hivyo fedha zinazotolewa na wafadhili zisaidie kutoa huduma stahiki kwa jamii ili kuponguza malalamiko ya wanananchi.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amewataka wadau wa afya kudumisha ushirikiano ili kuleta maendeleo katika kutoa huduma kwa jamii. Amesema kuwa umefika wakati sasa wadau wa afya kutoka Taasisi za Serikali na zisizo za kiserikali kuungana pamoja ili kufanya kazi kwa ushirikiano na kuongeza nguvu katika kutatua kero za afya kwa wananchi lengo likiwa ni kutoa huduma stahiki kwa jamii.

Alisema kuwa Taasisisi za Kiserikali na zisizio za kiserikali ziweke nguvu katika kutoa huduma za afya kuanzia ngazi ya vijiji, kata, Wilaya na Mkoa ili wananchi wapate huduma sawa na stahiki.

Wakati huohuo Mkurugenzi Mkapa Faundation Dr. Hellen Mkondya ameiomba Serikali kutoa vipaumbele vya sekta ya afya kwa wafadhili ili kutekeleza miradi inayoendana na matakwa ya wananchi.

Aidha, Dr. Donard Mmbando Mkurugenzi Health Link Initiatives ameipongeza Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na OR - TAMISEMI kwa kuandaa kikao cha ushirikiano kati ya Wadau wa afya na Serikali ili kujenga mahusiano ya pamoja na kuleta maendeleo kwa wananchi . Ameipongeza Serikali kwa kutoa miongozo, kuwezesha, upatikanaji wa huduma, uwezo ufikiaji wa huduma za afya za msingi lengo likiwa ni kutatua matatizo ya wananchi.

Aidha Semina hiyo ilihusisha wadau wa Sekta ya Afya ambao ni Mkapa Foundation, AMREF, Sikika, Itrahealth International, T-Marc Tanzania, Management and Development for Helth na mradi wa USAID boresha afya, Tanzania Youth Allience, Ingender Health, Tume ya Kikristo ya Huduma kwa jamii na Tanzania Health Support.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.