Serikali yasisitiza Utunzaji wa vyanzo vya maji

Serikali yasisitiza utunzaji wa vyanzo vya maji
--------------------------------------------------

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhge. George B. Simbachawene (Mb) amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha zinatunza vyanzo vya maji na miundo mbinu yake kwa maendeleo na afya bora ya jamii.

Mhe. Simbachawene ametoa agizo hilo alipokuwa akiongea na wananchi wa kijiji cha Chinyika wilayani Mpwapwa wakati wa ziara yake ambapo amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuchukua hatua za makusudi kulinda vyanzo vya maji na miundo mbinu yake kutokana na watu wasio waaminifu kuvamia vyanzo vya maji na kuharibu miundo mbinu yakiwemo mazingira ya vyanzo vya maji.

Amesema wapo watu waharibifu wa mazingira katika hamashauri nchini kama ilivyo kijiji cha Chinyika na kwamba atalisimamia suala hilo kwa karibu, “Ninajua kwamba waharibifu wa vyanzo hivi ni watu wenye nguvu lakini na mimi nitaongeza nguvu kwenye kikosi kazi cha Wilaya ili kuhakikisha kwamba wale wote wanaoishi karibu na vyanzo hivyo wanahamishwa na mazao yao yanaharibiwa, mifugo inaondolewa na wanapelekwa mahakamani” alisema Mhe. Simbachawene.

Athari zaidi zimethibitija katika Kijiji cha Chinyika na Lukole vilivyopo kata ya Chinyika kwa kukosa maji kutokana na Uharibifu uliofanywa na baadhi wa wananchi katika chanzo cha maji kwenye milima ya wota ambacho ndio chanzo kikuu cha maji ya mtiririko kwa wananchi zaidi ya elfu saba.

kutokana na uharibifu wa mazingira maeneo ya vyanzo vya maji wananchi wameendelea kulima, kufuga, kuchunga pamoja na kuishi katika maeneo hayo pasipo kuwa na shaka yoyote na kusababisha ukosefu wa maji kwa jamii inayotegemea vyanzo hivyo.

Pia aliongeza kuwa fedha za ukarabati wa miundo mbinu ya maji kutoka katika milima ya Wota kupitia Kingiti hadi kufika Lukole, zimekwishatengwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 160 kwa ajili na Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa na zimeanza kugharamia utekelezaji wa mradi huu utakaokuwa na manufaa kwa wananchi na yeye ataongeza shilingi milioni 13 kwa ajili ya kuchimba kisima.

Kwa upande wake Mhandishi wa maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Bi. Apolonia Temu ameelezea sababu ya ukosefu wa maji katika vijiji hivyo kuwa ni pamoja na uharibifu wa mazingira, ongezeko la watu ukilinganisha na hapo awali na uchakavu wa miundo mbinu ambayo kwa sasa imeanza kukarabatiwa.

Mhe. Waziri Simbachawene ameendelea na ziara yake katika Jimbo la Kibakwe na kwa siku ya tatu ametembelea vijiji vya Lukole, Kingiti na Iyenge ambapo amefanya mikutano ya hadhara, amesikiliza kero za wananchi pamoja na kukagua miradi ya maendeleo.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.