Serikali yaagiza Miradi viporo ikamilishwe kabla ya Kuanzisha Miradi mipya

Nteghenjwa Hosseah

Serikali yaagiza Miradi viporo ikamilike kabla ya Kuanza kwa miradi mipya

Serikali imetoa agizo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha inakamilisha miradi ya maendeleo wanayoitekeleza badala ya kuanzisha miradi mingine mipya na kusababisha kutokamilika kwa miradi.

Mhe.Simbachawene ambaye pia ni Mbunge wa Kibakwe ameyasema hayo katika ziara yake aliyoifanya jimboni Kibakwe katika vijiji vya Chinyika, Chaludewa na Fufu kwa kuagiza Halmashauri zote nchini kuzingatia ukamilishaji wa miradi iliyoanzishwa kabla ya kuanza kwa miradi mipya.

"Natoa Agizo kwa Halmashauri zote Tanzania kuhakikisha miradi yote iliyoanzishwa na wadau, nguvu za wananchi au Serikali kuhakikisha inakamilika kabla ya kuanzisha miradi mipya kupitia njia hii thamani ya fedha itaonekana,tofauti na hapo fedha zilizotumika zitapotea bila kusaidia jamii", Alisema Mhe.Simbachawene.

Mhe.Simbachawene amekemea kuwepo kwa hulka inayoendelea kukua katika Halmashauri nyingi nchini kuanzisha Miradi mipya ya maendeleo ili hali miradi viporo ikiendelea kuzorota kwa miaka mingi bila kukamilika huku ikiharibika na kusababisha upotevu wa fedha zilizowekwa hapo awali kama ilivyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa alipotembelea kijiji cha Chinyika Kata ya Mlunduzi, Tarafa ya Rudi ambapo alikuta baadhi ya miradi kutokamilika kutokana na kutotengewa fedha katika Bajeti ya mwaka wa fedha uliofuata.

Akiwa kijijini Chinyika, Mhe.Simbachawene alisema ni vyema miradi inayofadhiliwa na Wadau na ile ya Halmashauri kuwa na umiliki (ownership) na kuthamini nguvu na fedha zilizotumika ili hata ikiishia katikati Halmashauri husika ama wananchi wa eneo hilo kuwa na moyo wa kuendelea kutenga fedha au kuchangia kutoka mifukoni mwao na kukamilisha mradi husika.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri aliwasilisha changamoto za wananchi wa kijiji cha Chinyika kuwa ni pamoja na sintofahamu ya mapato ya mnara wa Halotel uliosimikwa katika kijiji hicho lakini hakinufaiki na pato lolote, pia baadhi ya wananchi kushiriki kwenye kilimo haramu cha zao la bangi na wakazi wachache kuharibu chanzo cha maji hivyo kusababisha ukosefu wa maji kwa wananchi wote.

Mhe.Simbachawene ameahidi kuongeza nguvu katika operesheni ya kuwakamata wale wote wanaolima zao haramu la bangi katika Jimbo la Kibakwe na kuwapeleka mahakamani kwa yeyote atakayekamatwa lakini pia wanaoharibu chanzo cha maji watashughulikiwa kisheria.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.