Dkt. Chaula atoa pongezi kwa Mfuko wa Pensheni wa PPF

Na. Sylvia Ernest , 22-07-2017

Dkt Chaula Atoa Pongezi kwa Mfuko wa PPF

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( OR-TAMISEMI) anayeshughulia afya Dkt. Zainabu Chaula ametoa wito kwa wadau wote nchini kuendelea kuwa mbele katika kuchangia maendeleo ya jamii hususan katika utoaji wa huduma ya afya kwa manufaa ya nchi nzima.

Dkt. Chaula ametoa rai hiyo wakati wa kukabidhiwa kwa vitanda 2 vya kujifungulia, vitanda 5 vya wodini ,magodoro 5 na mashuka 50 kutoka kwa Mfuko wa Pensheni wa PPF hafla iliyoambatana na uandikishwaji wa mfumo maalum wa kuchangia (WOTE SCHEME) unaoratibiwa na PPF katika viunga vya hospitali ya Mkoa Dodoma ,Leo. Katika hafla hiyo Dkt. Chaula aliupongeza mfuko huo kwa kuendelea kuchangia katika maendeleo nchini na kuongeza kuwa ni wito wa kila mmoja kuchangia katika maendeleo ya Taifa na kila mmoja anaalikwa kutumia fursa zilizopo katika maeneo yanayomzunguka ili kuchangia maendeleo ya nchi hususan katika sekta ya afya ambapo kuna upungufu mkubwa wa miundombinu na vifaa tiba.

‘’ Nawapongeza sana Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa kundelea kuchangia katika maendeleo ya nchi na natoa wito kwa wadau wengine kuendelea kujitokeza kwa wingi ili tuweze kutoka katika hatua moja kwenda nyingine kwasababu bado tuna changamoto katika maeneo mengi nchini” Aidha alitoa rai kwa wananchi kuendelea kujiunga na WOTE SCHEME unaoratibiwa na mfuko huo ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali kupitia mikopo inayotolewa pindi utakapojiunga na mfuko huo katka kukuza shughuli mbalimbali za kiuchumi na jamii

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma , Bi. Rehema Mndeme amesema kuwa ili mtoa huduma aweze kuhudumia wananchi kwa umakini zaidi lazima kuwepo na miundombinu iliyoboreshwa hivyo alitoa pongezi kwa mfuko huo kuendelea kuchangia katika maendeleo ya jamii na kuhamisha wananchi kujiunga na mfuko wa PPF.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma Dkt. James Charles ametoa pongezi kwa Mfuko wa Pensheni wa PPF kuendelea kutambua umuhimu wa kusaidia Taifa hasa katika sekta ya afya na kuhaidi kutunza vifaa hivyo kwani vina mchango mkubwa katika boresha utoaji wa huduma katika hospitali hiyo. Naye Mkurugenzi Mkuu Mfuko wa Pensheni wa PPF Bw. William Erio amesema kuwa mfuko huo umetoa misaada kwa kutambua kuwa kila mtanzania anatakiwa kuwa na afya nzuri ili waweze kufanya kazi za kiuchumi na kijamii na kuongeza kuwa kila mtoa huduma anatakiwa kukaa katika mazingira rafiki pale anapohudumia wananchi .

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.