Waziri Simbachawene Aitaka Manispaa Kuendeleza Miradi iliyoachwa na CDA.

Na Shani Amanzi.

Manispaa kuendeleza miradi ya CDA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ameitaka Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kuendeleza miradi iliyokuwa inafanywa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) na kufanya kazi kwa ueledi na umakini kwa kuwa Dodoma ni makao makuu ya nchi hivyo inahitaji kuwa jiji lililopangwa na lenye yenye miundombinu ya kisasa.

Waziri Mhe. Simbachawene aliyazungumza wakati wa ziara yake aliyoifanya leo mjini Dodoma wakati anatembelea miradi iliyokuwa inatekelezwa na CDA ambayo hivi sasa imekabidhiwa kwa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma. Alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli aliivunja Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma kutokana na mamlaka hiyo kuwa na migogoro na migongano na Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma na hivyo kuamua usimamizi na uendelezaji wa mji wa Dodoma kuwa sehemu moja kwa lengo la kuboresha tija na uwajibikaji.

Aliitaka Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kuyaboresha majengo ya Magorofa yaliyojengwa katika eneo la Kikuyu kwa kuweka madirisha ya vioo, kuweka maegesho ya kisasa ya magari kwakuwa wapo wahamiaji wengi kutoka maeneo mbalimbali waliohamia Dodoma wanaohitaji nyumba za kuishi.

“Natambua kuna upungufu wa watumishi katika Idara ya Ardhi na natambua shughuli ya upimaji wa Ardhi na Viwanja ni kubwa hivyo suala la kuajiri watumishi wapya ni muhimu na tutaiomba Tume ya Ajira itoe kibali cha kuwezesha kuajiriwa kwa wataalamu hao ili kuweza kuifanya kazi hiyo vizuri”alisema Simbachawene.

Mhe. Simbachawene alisema kwasasa anataka suala la vifaa, magari pamoja na nyumba zilizokuwa chini ya CDA ambazo kwa sasa zipo chini ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma ziendelee kubaki kama zilivyo mpaka pale litakapotolewa tamko kutoka serikalini. Aliitaka Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kuendelea kuboresha mashamba na misitu ili yasivamiwe na wananchi kwa kufikiria kuwa kwakuwa CDA imevunjwa basin a mambo mengine yamekuwa.

Katika ziara hiyo Mhe.Simbachawene alitembelea nyumba za magorofa ya Kikuyu, Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za bei nafuu katika eneo la Kizota, Kitalu cha miche ya Miti na Matunda cha Mailimbili, eneo la bandari Kavu Ihumwa na baadaye aliongea na wafanyakazi waliokuwa chini ya CDA na wale wa Manispaa ya Dodoma na kutoa maagizo mbalimbali.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.