Kituo cha Afya Rudi Wilayani Mpwampwa Kupatiwa Watumishi wapya

Na. Shani Amanzi


Katibu Mkuu TAMISEMI Eng Mussa Iyombe aagiza utoaji huduma bora kwa Wananchi

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Mussa Iyombe amewataka watumishi wa Halmashauri za Mji na Wilaya ya Korogwe kubadilika na kuboresha utendaji kazi wao kwa kutoa huduma bora kwa wananchi.

Katibu Mkuu Iyombe alitoa agizo hilo wakati wa kikao kazi alichokifanya katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe wakati wa ziara maalum ya kutembelea Halmashauri ya Mji wa Korogwe na Halmashauri zake ili kujionea utendaji kazi na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi .

Katika kikao hicho Katibu Mkuu Iyombe amepokea taarifa kutoka kwa Wakuu wa Idara mbalimbali za halmashauri za mji na wilaya na pia alitumia nafasi hiyo kutoa maagizo maalumu kwa watendaji hao ya kuwataka wabadilike na kuboresha utendaji wao sambamba na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama Tawala(CCM) inayosisitiza juu ya utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Aliwataka watumishi wanapotekeleza majukumu yao kukumbuka kuwa wao ni watumishi wa wananchi na hivyo kila mara kuhakikisha kuwa wanawatumikia vema wananchi. Aidha, aliwataka watumishi hao kujipima na kuona kama wanawahudumia wanachi vema kama inavyopaswa na pale ambapo hawafanyi vema kurekebisha hali hiyo ili wananchi waweze kupata huduma stahiki ambapo baada ya kikao hicho alitembelea baadhi ya miradi ya maendeleo yanayotekelezwa .

Mhandisi Iyombe aliwaagiza watumishi hao kuwahimiza wananchi kuendelea kujitolea na kushiriki katika kujiletea maendeleo yao kwa kuchangia nguvu kazi na mali.

Kikao kazi hicho kilihudhuriwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Bibi, Zena Said, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Robert Gabriel Ruhumbi, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe Mhe. Hilary Ngonyani pamoja na Watumishi wa Halmashauri za Mji wa Korogwe na Halmashauri ya mji wa Korogwe.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.