Mh.Naibu Waziri Jafo Awaagiza Waganga wakuu wa Mikoa na MSM kufanya kazi kwa uadilifu

Na. Shani Amanzi

Mheshimiwa Naibu Waziri Aagiza Waganga Wakuu wa MSM Kufanya kazi kwa uadilifu

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) ,Mhe. Selemani Jafo amewataka waganga Wakuu wa Mikoa na wilaya kufanya kazi kwa kufuata misingi na kanuni za kiutendaji na kuacha mazoea ili kuboresha sekta ya Afya Nchini.

Mhe. Jafo alitoa rai hiyo mapema leo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya juu ya maadili na uwajibikaji mahala pa kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano LAPF Mjini Dodoma. " Huduma bora za Afya ni moja ya njia ya kumhakikishia mwananchi haki ya kuishi, hakuna budi kuwepo kwa watumishi wenye kuzingatia kikamilifu misingi ya maadili ya utumishi wa Umma"

Alisema kuwa Misingi na Mikakati inakwenda pamoja hivyo ili kufanikisha malengo na kuboresha Sekta ya Umma Nchini ni wito wa kila mmoja kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kufuata kanuni zinazomuongoza katika eneo lake la kazi . Aidha aliwataka Waganga hao kuhakikisha wanahimiza usafi kwenye Hospitali na Vituo vya Afya pamoja na kuweka nguvu za pamoja katika kutokomeza magonjwa ya milipuko Nchini.

Naye Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anyeshughulikia Afya ,Dkt Zainab Chaula amewataka waganga hao kuwajibika na kufanya kazi kwa pamoja ili kutimiza mikataba ya makubaliano katika kutimiza majukumu yao na kutumia rasilimali na miundombinu iliyopo katika kuboresha Sekta ya Afya Nchini . '' Ili tuweze kufanya kazi kwa pamoja na kufikia lengo lazima tushirikiane Tuwajibike ,tupeane mawazo na kusaidiaana,hatutaweza kufikia malengo tuliyojiwekea kama hatutashirikiana”

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ,Dkt . James Charles alisema kuwa kikao hicho kitawaongezea weledi na mafunzo yatakayosaidia katika utendaji kazi hao na kuishukuru Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kutoa mafunzo hayo.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.