Mh. Waziri Simbachawene Aishauri Serikali kuhusu mfuko wa barabara TARURA

Na. Shani Amanzi

Mheshimiwa Waziri atoa ushauri TARURA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Mh.George Simbachawene ameishauri serikali kufikiria upya mgawanyo wa mfuko wa barabara kutoka asilimia 30 zinazogawiwa kwa sasa kwenye barabara za miji,halmashauri na mikoa kutokana na umuhimu wa barabara hizo katika kukuza uchumi wa wananchi.

Mh.Simbachawene amesema hayo mjini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mjini(TARURA)uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha mipango ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa. Mh.Simbachawene alisema barabara za mjini na vijijini zina mtandao mkubwa sana kwani una jumla ya km 108,581 hivyo ni lazima sasa serikali ifikirie namna ya kuongezea fedha angalau asilimia 40 kwa ajili ya kuchochea maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi.

“Kwa sasa mgawanyo wa fedha katika mfuko wa barabara ni asilimia 30 na asilimia 70 wanapewa TANROAD,lakini ukiangalia umuhimu wa barabara hizi kwa kuchochea maendeleo ya wananchi wa kawaida ni mkubwa sana,hivyo basi nitoe rai kwa serikali kufikiria upya kuhusu mgawanyo huu wa fedha,kwani kwa kuongeza fedha za mfuko wa barabara kuwezesha wakala (TARURA) kutengeneza barabara nyingi zaidi “alisema.

Aidha Mh.Simbachawene aliainisha changamoto kadhaa zilizokuwa zinazikabili halmashauri na miji katika ujenzi wa barabara kuwa ni pamoja na kupatikana kwa wahandisi wasiofaa,matumizi mabaya ya fedha,usimamizi mbovu wa ujenzi,kubadilishwa kwa matumizi ya fedha za mfuko wa barabara vinavyoshabiliana baina ya barabara za halmashauri moja na nyingine lakini kwa sasa kwa kuanzishwa kwa wakala wa barabara vijijini na mijini kutasaidia kutatua changamoto hizo.

Katika uzinduzi huo Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa alisema chombo hicho cha kusimamia barabara kipewe uhuru wa kujiendesha chenyewe kwa kutokuingiliwa bila sababu za msingi kwani wananchi wana matarajio makubwa sana kwa uanzishwaji wa wakala huo pia watendaji katika wakala huo wafanye kazi kwa weredi na waache kufanya kazi kwa mazoea. "Kwa sasa wafanyakazi wengi kwa kuanzia watachukuliwa kutoka katika halmashauri na maeneo mbalimbali,hivyo ningependa kuwaasa wote mtakaochaguliwa msiende kufanya kazi kwa mazoea ,bali kafanyeni kazi kwa weredi mkubwa na kujituma ili kuwaletea maendeleo wananchi hasa wa vijijini "" alisema.

Wakala wa barabara za vijijini na mijini(Tanzania Rural na Urban Road Agency)kwa kifupi TARURA uliozinduliwa jana mjini Dodoma umeanzishwa kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya kiutendaji kuhusu mandeleo ya barabara za vijijini na mijini katika ujenzi ,matengenezo pamoja na manejimenti ya barabara hizo ambapo majukumu hayo hapo awali yalikuwa yakifanywa na mamlaka ya serikali za mitaa na idara ya miundombinu chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais TAMISEMI ,Mhandisi Mussa Iyombe ,Wakuu wa Mikoa yote ya Tanzania bara,Makatibu Tawala,Wakurugenzi wa Halmashauri na Wahandisi kutoka katika halmashauri hizo.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.