Kituo cha Afya Rudi Wilayani Mpwampwa Kupatiwa Watumishi wapya

Na. Shani Amanzi

Kituo cha Afya Rudi Mpwapwa Kupatiwa Watumishi Wapya 1

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kufanya uhamisho kwa watumishi wasiofanya vizuri katika kituo cha Afya cha Rudi na kuleta watumishi wapya ili kuboresha utoaji wa haduma katika Kituo hicho na kumuagiza Mganga Mkuu wa Wilaya kuwasilisha mpango wa kuboresha utendaji wa Kituo cha Afya cha Rudi.

Mhe. Waziri ametoa agizo hilo katika ziara yake ya siku moja ya tarehe 24/7/2017 ya ukaguzi wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Wilaya ya Mpwapwa pamoja na kukabidhi madawati kwenye Kata 4 za Kibakwe, Masa, Ipela na Luhundwe pamoja na kukabidhi gari la dharura la wagonjwa (Ambulance) kwenye Kituo cha Afya cha Rudi.

‘’ haiwezekani wananchi wakimbie kutibiwa kwenye kituo chao cha Afya lazima kutakuwa na mapungufu, kituo ni kikubwa lakini kina hudumia wananchi wachache tofauti na makadilio na sio kwamba hakuna maradhi bali wanakimbia huduma duni ya kituo hiki”

Alisema kuwa watumishi wa kituo ambao hawafanyi vizuri katika utoaji wa huduma wapelekwe kwenye vituo vingine na kituo hicho kipatiwe watumishi ambao watahudumia wananchi wanaoishi maeneo jirani ya kituo hicho ili kuondokana na changamoto ya wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma kwenye vituo vya jirani.

Aidha aliongeza kuwa gari la wagonjwa lililokabidhiwa kituoni hapo linapaswa kutoa huduma na kubakia katika Kituo cha Afya cha Rudi na sio vinginevyo na kumuagiza Mkuu wa Kituo cha Polisi (OCS) wa Chipogolo kukamata gari na dereva ikiwa wataenda kinyume na matumizi ya gari hilo.

‘’Gari hili kazi yake ni kubeba wagonjwa na sio gari la kusafiria, na litakaa kituoni hapa kwasababu linahudumia wagojwa katika kituo hiki na sio Mpwampwa, likionekana linaenda kinyume na matumizi yaliyokusudiwa dereva na gari vyote vikamatwe’’alisisitiza.

Kutokana na kukosekana kwa daktari wa upasuaji katika Kituo cha Afya cha Kibakwe, Mheshimiwa Waziri aliamuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kuhakikisha kuwa daktari anafika haraka na kuanza kazi pamoja na stahili zake zipatikane na kuagiza kuwa kiasi cha shilingi milioni 790 zilizotengwa kwa ajili ya ukarabati zitumike kukarabati jengo la wagonjwa wa nje (OPD).

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.