Mh.Waziri Aagiza Kufanya tathmini ya uwiano wa madawati kwa wanafunzi

Na. Shani Amanzi

Serikali yaagiza Tathini ya Madawati na Wanafunzi nchini 1

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene amezitaka Halmashauri zote Nchini zifanye upya tathmini kati ya uwiano wa wanafunzi na madawati ili kupata uhalisia uliopo na kutoa taarifa kamili ya madawati yaliyopungua.

Mhe. Waziri ametoa agizo hilo alipofanya ziara ya siku moja kukagua Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya ya Mpwapwa pamoja na kukabidhi madawati 120 kwenye Shule zianazoonekana kuwa na upungufu mkubwa katika Kata 4 za Kibakwe, Masa, Ipela na Luhundwe pamoja na kukabidhi gari la dharura la wagonjwa (Ambulance) kwenye Kituo cha Afya cha Rudi.

“ Halmashauri zote Nchini zinatakiwa kuja na taarifa sahihi ya idadi ya madawati iliyopo ukilinganisha na mahitaji vinginevyo tutadanganyana kwamba madawati yapo mengi lakini kumbe baadhi ya watoto wanakaa chini” alisisitiza Mhe. Simbachawene

Alisema kuwa taarifa zinaonesha kuwa changamoto ya madawati imetatuliwa kwa kiasi kikubwa lakini kuna baadhi ya shule zina upungufu mkubwa wa mdawati na baadhi ya Mikoa wana madawati mengi lakini hayajafika kwenye shule zenye upungufu huo hivyo ni jukumu la Halmashauri zote kufanya tathmini upya kujua upungufu wa madawati uliopo na kuhakikisha kuwa madawati yaliyopo yanafika mashuleni.

Aidha katika ziara hiyo Mhe. Waziri ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 4, mabweni 2, matundu 34 ya vyoo na ukarabati wa maabara katika Shule ya Sekondari Kibakwe na kumuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kuwa ifikapo tarehe 17.07.2017 ujenzi wa mabweni uwe umekamilika.

‘’Tunajiandaa kupokea wanafunzi wa kidato cha tano naomba ifikapo tarehe 17.07.2017 ujenzi huu uwe umekamilika , Mkurugenzi naomba usimamie hilo” Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kibakwe Bw. Nikupala Sajigwa ameishukuru Serikali kwa kutoa kiasi cha shilingi 285,400,000/ kwaajili ya ukarabati wa miundombinu katika Shule hiyo na jeshi la magereza ambalo limekubali kujenga bweni moja na kufyatua tofali za ujenzi kwa gharama nafuu.

Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Waziri alikagua ujenzi wa nyumba ya mwalimu ya Shule ya Msingi Iyenge, ujenzi wa Chumba cha Upasuaji cha Kituo cha Afya cha Kibakwe, ujenzi wa Madarasa 4 na Mabweni 2 ya Shule ya Sekondari Kibakwe , kukabidhi madawati katika Kata 4 za Kibakwe, Masa, Ipela na Luhundwe yaliyotolewa na Coca Cola pamoja na kukabidhi gari la dharura la wagonjwa (Ambulance) kwenye Kituo cha Afya cha Rudi.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.