Serikali yawaasa Wadau Kutafuta Ufumbuzi Mabadiliko Tabianchi

Na. Shani Amanzi

Serikali yawaasa Wadau Kutafuta Ufumbuzi Mabadiliko Tabianchi

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi.Amina Shaaban amewataka Wafanyakazi wa Serikali na Wadau wa Mradi wa Kuhimili na Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi kuweza kupata ufumbuzi wa changamoto kubwa ya rasilimali katika mabadiliko ya tabianchi.

Bi.Amina Shaaban ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha Kamati ya Uongozi (Steering Committee) cha Mradi wa Kuhimili na Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi. Bi.Shaaban amesema kuna kiwango kidogo cha rasilimali ukilinganishwa na ukubwa wa athari za mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi.

Bi Shaaban ameishukuru Serikali ya Uingereza nakusema, “kupitia mashirika yake ya maendeleo kwa ufadhili ambao wameendelea kutoa katika mradi huu ili kufikia malengo yake ikiwemo Shirika la Msaada la Uingereza(UKAID), Taasisi ya Kimataifa ya Mazingira na Maendeleo (IIED) na Mwakilishi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo (UNCDF)”.

Naye Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kisekta Ofisi ya Rais TAMISEMI Dr. Andrew Komba amesema, ”kwa sasa mradi unatekelezwa katika Halmashauri 3 za wilaya za Ngorongoro, Monduli na Longido, zikiwa ni sehemu za Halmashauri za kuanzia utekelezaji wa mradi na tunalenga kufikia halmashauri nyingine zilizoathirika na mabadiliko ya tabia nchi“.

Kikao hicho ni cha kwanza cha Uongozi wa Mradi huo wa Kuhimili na Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia nchi (Decentralized Climate Financing Project) ambapo lengo kuu ni kujadili taarifa ya utekelezaji wa mradi, zikiwemo taarifa za fedha.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.