Serikali yashauri Vijana kuwa Wabunifu Kujipatia kipato

Na Shani Amanzi

Serikali yashauri Vijana kuwa Wabunifu Kujipatia kipato

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo amewataka vijana wa Taasisi ya Maendeleo ya Vijana Dodoma kuongeza ubunifu ili waweze kuwa washindani katika soko la biashara kwa kutumia fursa ya wahamiaji wanaokuja Dodoma.

Mhe.Jafo aliyasema hayo alipokuwa akikagua miradi ya Taasisi hiyo mapema leo na kuwataka kuwekeza kwenye kilimo kilimo cha mboga mboga na matunda kwani kinalipa.

’’Kumekuwa na tabia ya vijana kuchagua kazi na baadhi yao kusubiri kupata ajira kutoka Serikalini lakini nyie mmetoa mfano badala ya kutegemea ajira, mmejiajiri na nitahakikisha baadhi ya Wabunge wanakuwa wa kwanza kuja kununua matofali hasa kwa wale wanaojenga Dodoma ’’

“Nitaongea na Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma ili mpatiwe milioni moja kutoka katika Mfuko wa asilimia 5% ya makusanyo ya Manispaa ya Mapato ya vijana na milioni kumi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na mimi nachangia kwa kununua matofali mia tano “, alisisitiza Mhe.Jafo.

Naye Afisa Mipango na Mhasibu wa Taasisi ya DOYODO Bw.Elias Mbogo amesema taasisi inajipatia kipato chake kupitia vyanzo mbalimbali ikiwemo ada ya uanachama, tozo, miradi yao na misaada kutoka kwa Wadau wa Taasisi.

Taasisi ya DOYODO imesajiliwa kisheria mwaka 2002 na kuanza kufanya shughuli zake rasmi toka 2015 na miradi waliyonayo ni mradi wa matofali, mafunzo ya ziada kwa wanafunzi (tuition), ufundi chelehani na kukodisha ukumbi kwa ajili ya semina na sherehe mbalimbali.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.