Serikali Kudhibiti Matumizi ya Fedha za Miradi

Na Enock Mhembano


Serikali Kudhibiti Matumizi ya fedha za Miradi

Serikali imesema itatekeleza kwa ufanisi na kwa wakati Miradi yote ya Elimu ya Msingi na Sekondari nchini itakayofadhiliwa katika mwaka wa fedha 2017/2018 kwa fedha za Serikali pamoja na fedha za Wahisani mbalimbali kutoka nje.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu Bw. Tixon Nzunda, alipokuwa akizungumza katika kikao cha Kamati ya Maendeleo ya Elimu kilichofanyika katika Ofisi za Wizara mjini Dodoma.

“Serikali ya awamu ya Tano inawakaribisha Wadau wote wa maendeleo kuchangia fedha zao huku wakiwa na uhakika kwamba fedha hizo zitatumika katika miradi kama ilivyopangwa na miradi itatekelezwa kwa wakati”, Alisisitiza Bw. Nzunda.

Akichangia mada iliyohusu utekelezwaji wa miradi ya elimu katika kikao hicho kilichohudhuliwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo, Mashirika yanayochangia maendeleo ya elimu Nchini pamoja na wadau mbalimbali wa Elimu, Bw. Nzunda amesema kuwa fedha zote zitakazotolewa na serikali pamoja na wadau wa maendeleo ya Elimu Nchini zitatumika kama inavyotakiwa.

Ikumbukwe kuwa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ndio Wizara iliyo na jukumu la kusimamia utekelezaji wa sera za maendeleo ya elimu ya Awali, Msingi na Sekondari nchini.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk Leonard Akwilapo ambaye pia Mwenyekiti wa kamati ya Elimu alisema elimu nchini bado inakabiliwa na changamoto kadhaa na endapo wahisani wataendelea kujitolea kutoa fedha, basi changamoto hizo zitaendelea kupungua kwa kiasi kikubwa.

“kwa mfano, mfumo wa School Information System (SIS) ukiweza kufanikiwa nchi nzima katika mikoa yote, Serikali itakuwa na uwezo wa kupata taarifa muhimu za kila siku kuhusu, ni watoto wangapi wapo shule, shule ina walimu wangapi, walimu wangapi wamehama shule moja kwenda nyingine nakadhalika, hivyo fedha bado zinahitajika kutatua changamoto za namna hiyo” alisisitiza Dkt. Akwilapo.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.