Makamu wa Rais afungua Mashindano ya Umisseta Mwanza

Makamu wa Rais afungua Mashindano ya Umisseta Mwanza

Makamu wa Rais a Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amefungia mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi na Sekondari (UMISSETA na UMITASHUMTA) na kuiagiza mikoa na wilaya kuhakikisha kuwa masomo ya Haiba na Michezo na stadi za kazi yanafundishwa kikamilifu.

Akifungua mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Mhe.Samia pia ametaka mikoa na wilaya kutenga fedha za kuendeshea michezo.

Alisema kuwa mashindano hayo yanatoa fursa kwa washiriki kuonyesha vipaji mbalimbali walivyo navyo vya kimichezo na hivyo kuwapa fursa wadau mbalimbali wa michezo nchini kuona vipaji hivyo na kuwapa fursa ya kuviendeleza.

Mashindano ya mwaka huu yanashirikisha michezo ya mpira wa miguu kwa wavulana na wasichana, mpira wa kikapu kwa wasichana na wavulana, mpira wa mikono wasichana na wavulana, mpira wa wavu kwa wasichana na wavulana.

Michezo mingine ni Netball, riadha kwa mbio fupi, mbio za kati na mbio ndefu, mitupo na miruko.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.