Naibu Waziri aipongeza Nyamagana kutekeleza maagizo ya Serikali

Naibu Waziri aipongeza Nyamagana kutekeleza maagizo ya Serikali

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe.Selemani Jafo Halmashauri ya Wilaya ya Nyamagana kwa kutekeleza maagizo ya serikali kwa maslahi mapana ya wananchi.

Mnamo mwezi Februari, mwaka huu Jafo alitembelea wilaya ya Nyamagana ambapo licha ya kuongea na watumishi alitembelea pia miradi ya maendeleo na kutoa maagizo mbalimbali.

Miongoni mwa miradi hiyo ni ujenzi wa barabara za lami zinazojengwa chini ya ufadhili wa Benki ya dunia pamoja na kukagua miundombinu na utoaji wa huduma katika kituo cha afya cha Nyamagana.

Katika ziara yake, alitoa maagizo mbalimbali ambayo alitaka yatekelezwe Kabla ya mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.

Hata hivyo, jana baada ya kufanikisha zoezi la ufunguzi wa mashindano ya UMISETA yaliyozinduliwa rasmi na Makamu wa Rais Mheshimia Samia Suluhu Hassan, Naibu Waziri amefuatilia utekelezaji wa maagizo hayo na kukuta viongozi na watendaji wa jiji la Mwanza wametekeleza kwa kiwango cha kuridhisha.

Katika ujenzi wa barabara ijulikanayo kwa jina la Tilapia road, Jafo amekuta barabara ya lami imekamilika na kubakia maeneo madogo sana ya kuweka taa za barabarani.

Katika Kituo cha Afya cha Nyamagana, Naibu Waziri Jafo amekuta agizo la kuwekwa kwa mifumo ya kukusanya mapato kwa njia ya kielektroniki ukiwa umekamilika na mapato yameanza kuongezeka kutoka sh. milion 4 hadi Sh.milioni 10 kwa mwezi.

Mbali na hilo, pia amekuta wamekamilisha kutenga eneo Maalum kwa wagonjwa wa bima ambapo katika eneo hilo la bima mapato yameongezeka kutoka wastani wa Sh.milioni 6 hadi zaidi ya Sh.milioni 10 kwa mwezi.

Kufuatia utekelezaji huo, Jafo amewapongeza viongozi wote wa Nyamagana akiwemo Mkuu wa wilaya, Mbunge, madiwani pamoja na timu ya watendaji wa jiji la Mwanza huku akiwataka watendaji hao kuchapa kazi ili kuleta maendeleo kwa wananchi.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.