Wakurugenzi wa Halmashauri kubanwa

01-06-2017

Wakurugenzi wa Halmashauri kubanwa

Serikali imesema inampango wa kupeleka bungeni marekebisho ya ya fedha za serikali za mitaa, kwa lengo la kuwabana wakurugenzi watendaji wa halmashauri nchini kurejesha asilimia 20 ya mapato kwa vijiji.

Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Suleimani Jafo, alipokuwa akijibu swali la Flateri Massay(Mbulu Vijijini- CCM) Kaatika swali lake mbunge huyo alitaka kujua serikali ina mpango ganI wa kuwalipa posho au mishahara wenyeviti wa vijiji na vitongoji ili kurahisisha ufanisi wa kazi zao.

Alisema baadhi ya wakurugenzi watendaji wa halmashauri nchini wamekuwa wazembe kupeleka fedha hizo, lakini kuanzia sasa serikali itasimamia kikamilifu mchakato huo.

Jafo akijibu swali hilo, alisema sheria hiyo itakuwa ni mwarobaini kwa wakurugenzi wasiorejesha fedha hizo ambazo zinatumika pia kuwalipa posho viongozihao. “Hii sheria sasa itawalazimisha wakurugenzi kurejesha hizo fedha ili kuwanufaisha walengwa na itaweka utaratibu mzuri wa kuzirejesha” alisema.

Aidha, alisema serikali imeimarisha mifumo ya makusanyo ya mapato ya ndani ya halmashauri zote ili kujenga uwezo wa kutenga asilimia 20 kwenda kwenye vijiji. Alisisitiza kuwa serikali inathamini na kutambua kazi kubwa na nzuri inayofanywa na wenyeviti wa vijiji na mitaa katika maendeleo ya taifa.

Mheshimiwa Jafo alibainisha asilimia 17 ya fedha hizo zinatakiwa kutumika kwa shughuli za utawala, ikiwemo kulipa posho ya viongozi hao na asilimia tatu kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.