Tumieni Mafunzo hayo kuleta maendeleo katika wilaya zenu

Shani Amanzi

Tumieni Mafunzo hayo kuleta maendeleo katika wilaya zenu

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe amewataka Wakuu wa Wilaya 20 waliopata mafunzo nchini China kuhakikisha wanayafanyia kazi maarifa hayo na kutumia weledi huo kuleta maendeleo katika Halmashauri zao.

Mhandisi Iyombe alitoa rai hiyo katika kikao cha kuwasilisha taarifa ya mafunzo ya Wakuu wa Wilaya 20 yaliyofanyika nchini China kuanzia tarehe 30/4/2017 hadi 20/5/2017 kilichofanyika katika ofisi za Tamisemi Mjini Dodoma.

"Kila mshiriki ahakikishe maarifa na weledi alioupata unaleta mabadiliko chanya katika Mkoa na Halmashauri yake ili maarifa hayo yaweze kuwafikia watu wote na kuhamasisha maendeleo katika Mikoa yenu, " alisema

Alisema baada ya kupata mafunzo hayo Serikali inategemea mabadiliko katika Mikoa na Halmashauri zote nchini na kila Mkuu wa Wilaya atapimwa kwa kuonesha amefanya nini katika Mkoa na Halmashauri baada ya kupata mafunzo hayo.

Aidha Katibu Mkuu ametoa shukrani za pekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuridhia mafunzo haya kwa ajili ya Wakuu wa Wilaya na kuongeza kuwa mwelekeo wa Mheshimiwa Rais unaenda sambamba na jitihada za maendeleo zilizofanyika Nchini China.

Kwa upande wake Bi. Isabela Chilumba ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Nyasa na kiongozi wa msafara wa mafunzo hayo ameiomba Serikali kuboresha miundombinu na swala zima la utalii kwani lina matokeo chanya kwa maendeleo mengine yote ya kiuchumi nchini na kuwaomba viongozi wanaokwenda nje ya nchi wawe sehemu ya kutangaza utalii kwani ni jukumu letu sote kutangaza utalii wetu.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) na Ofisi ya Rais, Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora iliandaa mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya 20 ambapo mafunzo hayo yalifanyika kwa ufadhili wa Wizara ya biashara ya Jamhuri ya watu wa China ,mafunzo hayo yalikuwa juu ya utawala wa Umma na maendeleo ya uchumi wa Tanzania (Local Public Administration and Economic Development).

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.