Serikali yatangaza ajira za walimu

Fred Kibano

Serikali yatangaza ajira za walimu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikaliza Mitaa( OR-TAMISEMI), George Simbachawene ametangaza ajira mpya kwa walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati kwa shule za sekondari na kuwataka kuripoti katika vituo vyao vya kazi walivyopangiwa mara moja.

Mheshimiwa Simbachawene amesema Serikali inaendelea kushughulikia upungufu wa walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati kwani kibali cha kuajiri kimeruhusu kuajiri walimu wapatao 4,129 walimu waliopatikana ni 3,081.

Amesema Serikali imeajiri walimu hao 3,081 ambao wamepangwa katika Halmashauri zote nchini kulingana na uhaba wa walimu katika shule husika lakini pia Upungufu uliopo katika shule 3,602 za sekondari za Serikali ni 26,026 sawa na asilimia 60.14, ya waalimu 43,248 wa Sayansi na Hisabati wanaohitajika.

Kwa upande wa walimu wa masomo ya sanaa alisema shule za sekondari za Serikali zina ziada ya walimu 7,463 sawa na asilimia 13.38, kwani walimu waliopo ni 63,240 kati ya 55,777 wanaohitajika.

Kutokana na ziada hiyo ya walimu wa masomo ya sanaa, tayari Serikali imeanza kuchukua hatua ya kuwahamishia katika shule za msingi ili kupunguza upungufu uliopo huko.

Aidha, amesema Serikali inaendelea kupokea maombi ya walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati kutoka kwa wahitimu waliomaliza mafunzo mwaka 2015 kurudi nyuma kwani bado inahitaji waalimu 1,048 ili kutimiza idadi ya walimu 4,129 waliotolewa kibali.

Amewataadharisha walimu ambao hawataripoti katika vituo ndani ya muda uliopangwa kuwa watafutwa na nafasi zao zitakuchukuliwa na wahitaji wengine.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.