Fanyieni kazi tafiti za asasi za kiraia

Shani Amanzi

Fanyieni kazi tafiti za asasi za kiraia

Serikali imewataka watendaji serikalini kuzifanyia kazi tafiti mbalimbali zinazotolewa na asasi za kiraia ili kuleta matokeo chanya na kuboresha maisha ya watanzania.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mheshimiwa Selemani Jafo amesema hayo wakati akipokea ripoti ya Takwimu Mpya za Uwezo Tanzania iliyopo katika TWAWEZA.

Amesema kuwa Watendaji Serikalini sasa wana budi wa kufanyia kazi tafiti mbalimbali zinazotolewa na Azaki za kiraia zinazolenga masuala yaliyopo katika jamii ili kuiwezesha serikali kuyafanyia kazi matokeo ya tafiti na kuboresha hali ya watanzania.

"Kwa matokeo haya ya Tafiti ya TWAWEZA kupitia Uwezo Tanzania ni kipimo tosha cha kutuonesha sisi kama viongozi yapi tunayotakiwa kufanya na yapi hatutakiwi kufanya na yapi tunatakiwa tuyarekekebishe katika sekta ya elimu na matokeo haya tutayafanyia kazi," Naibu Waziri alisema.

Aidha Mhe. Jafo aliwataka wabunge kutumia vikao muhimu vya kisheria kwenye maeneo yao ya kazi katika kuhakikisha matokeo ya tafiti yanasaidia kuboresha sekta ya elimu katika Halmashauri huku serikali ikiendelea kuwekeza katika sekta ya elimu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza Aidan Eyakuze alisema kuwa tathmini hii inayopima matokeo ya kujifunza ambayo ambayo ni kubwa barani afrika inayotekelezwa kwenye baadhi ya nchi ikiwamo Kameruni, Nigeria, Senegali,Mali, Ghana na Burkina Faso inasaidia kuonesha hali halisi ya iliyopo mashuleni ili kuboresha sekta ya elimu.

Naye Meneja wa Uwezo Tanzania Zaida Mgalla amewataka viongozi wa Serikali na wabunge kutumia tafiti hii ya uwezo katika kuhakikisha wanashiriki katika kuboresha elimu katika maeneo yao na Tanzania kwa Ujumla ikiwa ni lengo kuu la kuhahakikisha wanaifikisha sekta ya elimu pale inapotakiwa.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.