Kamati ya Bunge yaidhinisha makadirio ya Bajeti ya wizara

Na Fred Kibano

Kamati ya Bunge yaidhinisha makadirio ya Bajeti ya wizara

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) Mhe. George B. Simbachawene amewasilisha makadirio tarajiwa ya Bajeti yanayoihusisha Ofisi hiyo, Taasisi zilizo chini yake, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa baada ya kufanya mapitio na majadiliano ya pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa mjini Dodoma.

Akiwasilisha bajeti hiyo, Mhe. Simbachawene amesema katika mwaka wa fedha 2017/2018 makadirio ni shilingi 6,504,892,097,138.

"Katika Mwaka wa Fedha 2017/2018 Ofisi ya Rais TAMISEMI, Tume ya Utumishi wa Walimu, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa zinaombewa jumla ya shilingi 6,504,892,097,138," ambapo shilingi 1,935,733,406,643 ni fedha kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.

Aidha, Mhe. Simbachawene (Mb) amevitaja baadhi ya vipaumbele vya Bajeti katika mwaka wa fedha wa 2017/2018 ambavyo pia Kamati ilipendekeza kuwa ni, "kuendelea kuboresha mifuko ya Wanawake na Vijana na kuwawezesha Wananchi kushiriki katika shughuli za Maendeleo," pia kuendelea kuzijengea Halmashauri uwezo ili ziwe na uwezo mkubwa wa kukusanya mapato ya ndani na kuboresha usimamizi wa fedha na mali nyingine za Serikali kwa kuwapatia vitendea kazi na mafunzo stahiki.

Ameyataja makadirio ya makusanyo ya ndani Ofisi ya Rais TAMISEMI na Taasisi zake kuwa ni Shilingi 22,266,063,908, lakini pia makadirio ya makusanyo ya ndani na maduhuli yatakayofanywa na Ofisi ya Rais TAMISEMI, Taasisi zake, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Mwaka wa Fedha 2017/2018 yanatarajiwa kuwa shilingi 713,187,789,615.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.