Tovuti za Mikoa na Halmashauri zitoe taarifa kwa wakati

Na Shani Amanzi

Tovuti za Mikoa na Halmashauri zitoe taarifa kwa wakati

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe.George Simbachawene amezitaka Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwawezesha Maafisa habari waliopo chini ya Ofisi zao kutekeleza majukumu yao kwa wakati na haraka ili kuendana na kasi ya ukuaji wa kiteknolojia na kupashana habari ili kuwaletea Wananchi maendeleo.

Mheshimiwa Simbachawene ameyasema hayo mjini Dodoma wakati akizindua tovuti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ambazo zitatumika katika uwasilishaji wa habari na taarifa muhimu kwa Wananchi.

"Nawaagiza Wakuu wa Mikoa wote kuhakikisha Maafisa Habari katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa wanawanunulia vifaa hivi muhimu kama kamera, mtandao wa kompyuta, kompyuta na vinginevyo vya kufanyia kazi hizi muhimu ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa na kwa gharama ya ofisi ili waweze kuwapatia Wananchi taarifa ikiwa ni haki yao ya msingi ya kupata taarifa," alisema Mhe.Simbachawene.

Mhe.George Simbachawene amesema kwa kuwa Tanzania iliweka saini Azimio la 'Open Government Partnership' mwaka 2011, kuweka uwazi wa shughuli za Serikali kwa Wananchi, ikiwa na lengo la kuimarisha Utawala Bora,kuondoa rushwa na kujenga imani kwa Wananchi wake na Azimio linaweka msisitizo kwa Wananchi kupata taarifa kwa wakati na uhuru zaidi.

Aidha Mhe.Simbachawene amewataka Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri kuhakikisha kwamba tovuti zao zinakuwa na taarifa sahihi na za kutosha na zinatolewa kwa wakati.

Pia amewataka Watendaji katika Mikoa na mamlaka za Serikali za Mitaa kuondoa urasimu katika kutoa taarifa.

"Lazima taarifa zitolewe kwa wakati ili tovuti hizi zitumike kweli kwa malengo yaliyokusudiwa," alisisitiza Mheshimiwa Simbachawene.

Waziri Simbachawene aliwashukuru Watu wa Marekani kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani USAID kwa kuwezesha Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ambao kupitia ufadhili huo umeweza kuendesha mafunzo ya utengenezaji wa tovuti hizo.

Kwa upande wake Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe aliwataka Maafisa Habari kutowaangusha Wananchi katika kuwapa taarifa pasipo urasimu wowote.

Waziri Mwakyembe amewataka Maafisa Habari kuhakikisha kuwa tovuti hizo zisigeuke kuwa magofu ya habari bali majokofu kwa kupata habari mpya kila siku.

Katika mafunzo hayo, Maafisa habari, na Maafisa Tehama kutoka halmashauri 185 na Mikoa 26 walishiriki Mafunzo hayo na kufundishwa namna ya kuandaa taarifa mbalimbali katika tovuti zao.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.