E: DKT. CHAULA Azitaka Timu za Uwezeshaji wa Huduma za Afya Kutumia Vizuri fedha za Wafadhili

Na Rebeca Kwandu

Maelekezo ya Naibu Katibu Mkuu

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR-TAMISEMI) anayeshughulikia Afya,Dkt Zainabu Chaula amewataka wajumbe wa timu ya uendeshwaji wa huduma za Afya ngazi ya Mkoa na Wilaya, kutumia vizuri fedha za Mfuko wa Pamoja wa Wafadhili ( Health Basket Fund ) ili kuboresha huduma za afya nchini.

Dkt. Chaula alitoa agizo hilo alipozungumza na baadhi ya wajumbe wa timu ya uendeshwaji wa huduma za afya ,waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na waganga Wafawidhi katika hospitali za Rufaa na Mikoa juu ya upitiaji/uhakiki wa Mipango kabambe ya afya ya mwaka 2017/18 kwa kuhusisha ngazi ya Mkoa, Halmashauri na Wizara ya afya mjini Dodoma. “Tumieni hizo fedha kuboresha huduma za afya , zitumike kununua dawa na kuboresha miundombinu ya hospitali zetu nawaomba tusikae na hizo fedha wakati tunajua wazi vituo vyetu vya afya vina changamoto nyingi ambazo zinafanya huduma ya afya kuzorota, tumieni hizo fedha vizuri”

Aliongeza kuwa idadi ya wagonjwa katika hospitali za Serikali inazidi kupungua kwasababu wanahama na kwenda hospitali binafsi wakitoa sababu ya kukosa huduma bora, hivyo aliwataka wasifanye kazi kwa mazoea bali wafate kanuni na misingi ya utuaji wa huduma bora pamoja na kuboresha miundombinu na upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya na hospitali zote katika ngazi ya Mkoa na Wilaya.

‘’Hata kama hospitali inamajengo mazuri kama kanuni na misingi ya utoaji huduma bora haitafatwa basi sekta ya afya itaendelea kuzorota kila siku,ukosefu wa dawa unachangia kwa kiasi kikubwa kupotea kwa wateja wakiwemo wa NHIF/CHF,wanaona bora wakapate huduma katika vituo au hospitali binafsi kwasababu huduma zetu hazikidhi mahitaji yao” Kwa upande wake Kaiumu Mkurugenzi wa huduma za Tiba Wizara ya Afya, Dkt Doroth Gwajima amewataka wajumbe hao kujipima katika utoaji wa huduma bora katika ngazi za Mikoa ana Wilaya kwa kuangalia idadi ya wagonjwa wanahudumiwa katika vituo vya afya na hospitali zao na kuhakikisha kuwa hospitali zinakuwa katika hali ya usafi.

“ Jaribu kukaa na kujiuliza kwanini unapata wagonjwa wachache katika hospitali yako ,hospitali nyingine haziridhishi kwa kweli ,huduma mbovu mazingira machafu , ukiona unapata wagonjwa 10 kwa siku ujue una kasoro, jaribu kujitathimini uone una mapungufu gani mpaka ukimbiwe na wagonjwa “

Kikao hiko kilihudhuriwa na baadhi ya wajumbe wa timu ya uendeshwaji wa huduma za afya ,waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na waganga Wafawidhi katika hospitali za Rufaa na Mikoa katika Halmashauri 184 na Mikoa 26 kwa lengo la upitiaji wa mipango kabambe ya afya mwaka 2017/18 kwa kuhusisha ngazi ya Mikoa ,Halmashauri na Wizara ya Afya.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.