Kikao cha kazi

Na Shani Amanzi

Kikao cha kazi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa George Simbachawene akiongoza kikao cha pili cha Majadiliano baina ya Serikali na Viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania tarehe 16 Machi, 2017 mjini Dodoma. Waziri wa Nchi aliwasifu wajumbe wa kikao hicho kwa kuendesha majadiliano hayo kwa utulivu na akasisitiza umuhimu wa taasisi hizo kuendelea kukutana katika vikao hivyo katika siku za baadaye.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Bernard Makali, na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi,Teknolojia na Ufundi Profesa Simon Msanjila na Wakurugenzi wanaoshughulikia sekta ya Elimu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Elimu Sayansi,Teknolojia na Ufundi, Tume ya Utumishi wa Walimu na taasisi nyingine za Serikali . Wengine waliohudhuria kikao hicho ni Rais wa Chama cha Walimu Tanzania Gratian Mukoba,Katibu Mkuu wa CWT Yahaya Msulwa na Naibu Katibu Mkuu wa CWT Mwalimu Ezekiel Olouch.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.