Benki ya CRDB kutumia mfumo wa kielektroniki katika huduma za afya

Na Shani Amanzi

Benki ya CRDB kutumia mfumo wa kielektroniki katika huduma za afya

Benki ya CRDB tarehe 14 Machi, 2017 ilikutana na Uongozi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI ili kuelezea mpango wake wa kutoa huduma ya afya kwa kutumia kadi za kielektroniki ili kurahisisha utolewaji wa huduma hiyo na pia kuviwezesha vituo vinavyotoa huduma za afya kupata mapato yake moja kwa moja.

Waliokaa kuanzia kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais Tamisemi Bibi Susan Chekane, anayemfuatia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Shamata Shaame Khamis.

Kwa mujibu wa Meneja wa Biashara wa benki hiyo Bi May Ndunguru, mfumo wa Kieletroniki wa Huduma za Afya utamuwezesha mteja anayehitaji huduma ya afya kupata huduma hiyo kwa urahisi kwani taarifa zake zote zitakuwa zimeshachukuliwa na pale anapofika hospitalini kazi yake ni kupata huduma moja kwa moja kupitia Master Card.

Aliongeza kuwa mfumo huo utamsaidia mteja kupata huduma moja kwa moja hata kama ameugua ghafla pasipo kuwa na pesa mkononi kwa kuwa ana Master Card tayari ambayo ameshailipia na atapata huduma za kimatibabu kiurahisi.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.