Ziara ya Wajumbe wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi Dodoma

Na Mathew Kwembe

Ziara ya Wajumbe wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi Dodoma

Wajumbe wa Kamati ya Sheria, Utawala Bora na Idara Maalum wa Baraza la Wawakilishi wakiwa katika picha ya Pamoja na Maafisa wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa mjini Dodoma.

Waliokaa kuanzia kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa Ofisi ya Rais Tamisemi Bibi Susan Chekane, anayemfuatia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Idara Maalum Zanzibar Mhe. Shamata Shaame Khamis.

Anayemfuatia Naibu Waziri ni Mhe.Machano Othman Said, Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Utawala Bora Zanzibar, na kulia ni Mhe.Mwantatu Khamis Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Utawala Bora Zanzibar

Wajumbe hao kutoka baraza la Wawakilishi wapo katika ziara ya siku mbili mjini Dodoma ambapo walipata fursa ya kushiriki katika semina kuhusu majukumu, mahusiano na mawasiliano kati ya Serikali kuu na Mamlaka za Serikali za Mitaa, pia walipata fursa ya kuelezwa kuhusu dhana ya Ugatuaji Madaraka na pia Ukusanyaji wa Mapato kwa njia ya Mfumo wa Kielektroniki.

Tarehe 15/03/2017, wajumbe hao watapata fursa ya kutembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambapo watapata maelezo kuhusu uhalisia wa dhana ya Ugatuaji Madaraka kwa Umma na baadaye kuelekea Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma kwa ajili ya kuona utekelezaji wa dhana ya Ugatuaji na kuona hali halisi ya Ukusanyaji wa Mapato kwa njia ya Kielektroniki

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.