Waziri Simbachawene asisitiza usafi wa mazingira mjini Dodoma

Na Sylvia Hyera

Waziri Simbachawene asisitiza usafi wa mazingira mjini Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene amewataka viongozi wa Manispaa ya Dodoma kuwa wabunifu katika kushughulikia suala la usafi wa mazingira ili kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa kuvutia na wakati huo huo kuutokomeza ugonjwa wa kipindupindu.

Alisema ili waweze kutekeleza jambo hilo mapema wanatakiwa kuanza utekelezaji katika masuala yasiyohitaji fedha wake wakati wakitafuta fedha za kutekeleza mambo yanayohitaji fedha ili kuanza kufanya mabadiliko kwa haraka.

Akizungumza katika ziara fupi ya kutembelea maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma iliyokuwa na lengo la kuhamasisha utunzaji na usafi wa mazingira ya mji wa Dodoma ili kujikinga na kipindupindu katika maeneo ya River Pombe, Uwanja wa Barafu na katika Soko kuu la Majengo Mhe. Simbachawene alisema itakuwa ni aibu kuwa na kipindupindu katika mji wa Dodoma kwakuwa hivi sasa unapokea wageni mbalimbali kutoka nchini na nje ya nchi.

Mhe. Simbachawene aliwataka viongozi wa Mkoa wa Dodoma, Manispaa ya Dodoma na Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Makuu kushirikiana na kuhakikisha mazingira ya mji wa Dodoma yanakuwa safi likiwepo suala la kuifanyia mitaro usafi.

Alitaka uongozi wa Manispaa ya Wilaya ya Dodoma kuhakikisha wanaweka ulinzi katika eneo la Pombe River kwa kutumia Walinzi au Jumuiya ya watu waliojenga karibu na eneo hilo ili kulilinda na kuhakikisha wananchi hawatupi takataka katika.

Aliwataka wakazi wa Dodoma kujipanga kutumia fursa zinazojitokeza Dodoma kutokana na kuja kwa wageni wengi ili kujiongezea kipato lakini wakati huo huo kuhakikisha huduma wanazotoa zinazingatia ubora kwa kuwa safi.

Aidha aliwahakikishia wageni wanaohamia Dodoma kuwa Mamlaka ya Mkoa wa Dodoma na Manispaa zimejiapanga katikamkuhakikisha kuwa huduma za afya zinakuwepo wakati wote na kuwatoa hofu za kukosa huduma za afya.

"Serikali imejenga hospitali kubwa ya Benjamin Mkapa ambayo ubora wake kwa utoaji wa huduma Tanzania inaweza kuwa ya kwanza kwa kutoa matibabu ya daraja la Kwanza. Kituo cha Afya cha Makole pia kimeboreshwa na kupandishwa hadhi ambapo sasa kitatoa huduma za hospitali. Lakini pia vituo binafsi vya afya na hospitali ya DCMC vimejipanga kusaidiana na Serikali katika utoaji wa huduma za Afya," alisema Mhe. Simbachawene.

Naye, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Zainab Chaula amemtaka mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma kuhakikisha kuwa wafanyanya biashara ndogondogo wanahamia katika Uwanja wa Barafu ili kufanya shughuli zao katika eneo salama na safi kwa lengo la kutokomeza magonjwa ya milipuko ukiwemo ugonjwa wa kipindupindu.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.