Waziri Simbachawene ataka matumizi sahihi ya fedha za maendeleo

Na Mwajuma Ally

Waziri Simbachawene ataka matumizi sahihi ya fedha za maendeleo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene amewataka MakatibuTawala wa Mikoa kuhakikisha kuwa ofisi zao zinasimamia vema utunzaji na matumizi sahihi ya fedha za umma katika Mamlaka zilizo chini yao.

Akizungumza na Makatibu Tawala wa Mikoa mjini Dodoma jana, Mhe. Simbachawene amesisitiza umuhimu wa Viongozi hao kuzisimamia vizuri ofisi zao ili zijiepushe na changamoto mbalimbali za usimamizi mbaya wa fedha hasa unaohusu miradi ya maendeleo.

Mhe.Waziri alisema kuwa changamoto kubwa inayoikabili baadhi ya Mikoa ipo katika uendeshaji na usimamizi wa fedha inayopelekea upoteaji wa fedha za maendeleo ya halmashauri za mikoa husika.

Aidha Mhe.Simbachawene aliwataka Makatibu Tawala hao wa Mikoa kuwa washauri wakuu katika halmashauri zao hasa katika masuala ya uchumi na kilimo ili kuharakisha maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na kubuni vyanzo vipya vya mapato.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.