Serikali kushughulikia madai ya walimu kwa utaratibu

Na Sylvia Hyera

Serikali kushughulikia madai ya walimu kwa utaratibu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene amewataka walimu kuwa watulivu na wavumilivu wakati Serikali ikiendelea kushughulikia madai yao kwa utaratibu.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma mara baada ya kikao na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mhe. Simbachawene amesema kuwa Serikali imepokea madai hayo na kuahidi kuyafanyia kazi hivyo aliwataka walimu nchini kuwa watulivu wakati Serikali ikiendelea kushughulikia madai hayo.

"Sio kwamba Serikali hailipi madai ya walimu ,yanalipwa na yataendelea kulipwa niwaombe walimu wawe watulivu na wavumilivu, Serikali inatambua madeni hayo, inalipa na itaendelea kulipa madai hayo," alisema Mhe. Waziri

Pia Mhe. Waziri alitoa pongezi kwa walimu na kutambua mchango wao katika kuleta maendeleo , amewaomba walimu kutoa nafasi ili Serikali iendelee kushughulikia madai hayo japo kuwa hayawezi kuisha kwa mara moja lakini Serikali inatambua madai hayo na inaendelea kuyafanyia kazi.

Aidha Mhe. Waziri ameahidi kutengeneza utaratibu wa kukutana na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) mara kwa mara kuzungumza na kutatua changamoto mbalimbali zinazo wakabili walimu nchini ili kuleta maendeleo na kudumisha amani nchini.

Kwa upande wake Rais wa Chama cha Walimu Bw. Gratian Mukoba ameridhia mazungumzo ya chama hicho na Serikali na kukanusha habari zinazosambazwa na vyombo vya habari kuwa tarehe 01/03 ungefanyika mgomo kama ilivyotangazwa na vyombo vya habari nchini

Awali Chama cha Walimu nchini kupitia kwa bwana Mukoba waliitaka Serikali itatue changamoto na madai ya walimu nchini na endapo madai hayo kutotatuliwa 01/03 wangeanzisha mgogoro nchi nzima.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.