Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto yajenga jengo la kisasa

Na Mathew Kwembe

Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto yajenga jengo la kisasa

Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto iliyopo mkoani Tanga imefanikiwa kuondokana na kero ya muda mrefu ya kukosa jengo la utawala linalotosheleza mahitaji ya watumishi wake baada ya kukamilisha ujenzi wa jengo hilo baada ya kupata mkopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa.

Kwa mujibu wa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo bwana Jumanne Shauri, halmashauri hiyo hatimaye imeondokana na kero hiyo baada ya kuzitumia vyema shilingi milioni 400 ambazo walikopa kutoka Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa.

Alisema kiasi hicho pamoja na fedha zao za ndani zimewawezesha kukamilisha ujenzi huo, na hivyo kuiwezesha halmashauri hiyo kuwahudumia wananchi wake katika mazingira bora, nafuu na ya kisasa.

Bwana Shauri alisema kabla ya kuhamia kwenye jengo hilo watumishi wa Halmashauri hiyo walikuwa wamegawanyika katika ofisi mbalimbali za umma wilayani humo, na hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi waliokuwa wakihitaji huduma katika halmashauri hiyo.

Sambamba na hilo, gharama za uendeshaji hususani gharama za umeme, walinzi na maji zilikuwa kubwa kutokana na halmashauri kulazimika kutoa huduma hizo kwa watumishi wake na ofisi katika sehemu tofauti, suala ambalo halipo kwa sasa baada ya gharama hizo kuwa sehemu moja pekee.

"Tunawahudumia wananchi vizuri, na hawapati usumbufu kama zamani, kwani ukitaka kumuona Mkurugenzi au Mkuu wa Idara, wote utawapata katika jengo hili hili," alisema.

Bwana Shauri alizitaka halmashauri nyingine zinazotaka kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo kuitumia Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa kwa kuomba mkopo ambao una masharti nafuu kulinganisha na taasisi nyingine za kifedha nchini.

Pia aliiomba serikali kuiongezea nguvu ya kifedha Bodi hiyo ili iweze kukidhi mahitaji ya halmashauri mbalimbali zinazohitaji mkopo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo.

Kwa upande wake Mchumi wa halmashauri hiyo bwana Alfa Moshi alisema kuwa halmashauri hiyo ilifuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha Madiwani kupitia vikao vya baraza na kisha kuandika andiko ambalo lilipelekwa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa kwa ajili ya kuomba mkopo huo.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.