Ujenzi wa Hosteli ya Benjamin Mkapa jijini Mbeya

Ujenzi wa Hosteli ya Benjamin Mkapa jijini Mbeya
--------------------------------------------------

Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa imeikopesha Halmashauri ya jiji la Mbeya shilingi milioni 600 ili kujenga Hosteli kama mojawapo ya vyanzo vyake vya mapato.

Kukamilika kwa ujenzi wa hosteli hiyo kunafuatia kukamilika kwa mradi wa ukumbi mkubwa wa Benjamin Mkapa ambao pia ulijengwa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya baada ya kupata fedha za mkopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa

Akizungumzia mafanikio ya miradi hiyo, Katibu wa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa Bibi Apolonia Chagaka amesema kuwa jiji la Mbeya ni mfano mzuri wa namna halmashauri zinavyoweza kubuni miradi mizuri ya maendeleo ambayo inakuwa chanzo kikubwa cha mapato.

Amesema kuwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya limebuni kuwa na jengo la hosteli baada ya kuona kuwa jiji hilo limekuwa na upungufu mkubwa wa majengo yanayoweza kukidhi mahitaji ya hosteli kufuatia kuwepo kwa ongezeko kubwa la wananchi wanaohitaji huduma hiyo.

"Mathalani, kumekuwa na mahitaji makubwa ya majengo yanayoweza kutumiwa na wageni kwa malazi au huduma nyingine za kijamii, ndiyo maana wenzetu wa Mbeya wamejenga jengo hili ambalo kwa sasa linatumika kama hosteli na Ofisi kwa Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Mbeya," alisema

Kwa mujibu wa Bibi Chagaka, Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa iliona ni vema kuwapa fedha nyingine za mkopo uongozi wa jiji la Mbeya kufuatia kufanya vizuri kwa Mradi wa Ukumbi wa Benjamin Mkapa ambao ndiyo ukumbi mkubwa katika jiji hilo

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.