Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa yawezesha ujenzi wa Stendi ya Mabasi Mbinga

Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa yawezesha ujenzi wa Stendi ya Mabasi Mbinga
--------------------------------------------------

Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa imeikopesha Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga (sasa Halmashauri ya Mji wa Mbinga) kiasi cha shilingi 1.6 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi cha Mbinga.

Kwa mujibu wa Katibu wa Bodi hiyo ambayo ipo chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bibi Apolonia Chagaka, Mradi wa Stendi ya kisasa ya mabasi ya Mbinga ni mojawapo ya miradi ambayo ilipata fedha kutoka katika Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa na kwamba kituo hicho hivi sasa kinafanya kazi.

Alisema kukamilika kwa ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi ya abiria mbali na kutoa huduma kwa wananchi pia kinatarajia kuwa kitega uchumi kizuri kwa halmashauri ya mji wa mbinga.

Bibi Chagaka alisema mradi huo pia ulihusisha ujenzi wa majengo makubwa mawili ya ghorofa ambayo yatakuwa na ofisi mbalimbali ikiwemo ni pamoja na maduka.

Aidha Katibu huyo wa Bodi aliipongeza iliyokuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga sasa (Halmashauri ya Mji wa Mbinga) kwa namna walivyoandaa mradi huo na kusimamia ujenzi wake hadi ulipokamilika

Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Kikwete aliifungua rasmi stendi hiyo mnamo tarehe 20 Julai, 2014.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.