Manispaa ya Dodoma yapongezwa kukamilisha ujenzi wa Madarasa

Manispaa ya Dodoma yapongezwa kwa kukamilisha ujenzi wa Madarasa
--------------------------------------------------

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo ametoa pongezi kwa uongozi wa halmashauri ya Manispaa Dodoma na shule ya msingi Chang’ombe A kwa kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa wakati.

Mhe. Jafo ametoa pongezi hizo alipotembelea shule hiyo kukagua utekelezaji wa agizo alilolitoa hapo awali kuhusu ujenzi na ukarabati wa miundo mbinu katika shule ya Chang’ombe A ifikapo mwezi Januari mwaka huu ambapo ameridhishwa kwa hatua nzuri ya ukarabati na kukamilika kwa vyumba sita vya madarasa.

"Maagizo niliyoyatoa yalikuwa magumu sana lakini nia yangu ilikuwa kuwatengenezea mazingira rafiki wanafunzi na walimu, nimefarijika na utekelezaji wake, hali haikua nzuri hapo mwanzo lakini nimefarijika kwa kazi nzuri, muonekano wa madarasa unaridhisha nawapongeza sana" alisema.

Naibu Waziri amewataka wanafunzi na walimu wa shule ya msingi Chang’ombe A kutunza na kuitumia miundo mbinu hiyo rafiki vizuri ili kuongeza ufaulu katika shule hiyo na kuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa shule nyingine, alisema.

Naye Mwalimu Mkuu wa Chang,ombe A, Bi. Nelly Kinyaga ameishukuru Serikali kwa kuboresha miundombinu ya shule hiyo kwani awali mazingira ya shule hiyo yalikuwa sio rafiki kwa wanafunzi na walimu kutokana na upungufu wa matundu 20 ya vyoo na vyumba nane vya madarasa.

" Kwa kweli kulikuwa na changamoto sana wanafunzi walikua wengi na madarasa machache lakini kwa sasa hatuna watoto wanaokaa chini na msongamano wa wanafunzi darasani umepungua kwa kiasi kikubwa, naishukuru Serikali na Mhe. Jafo kwa kutilia mkazo ukarabati wa miundo mbinu ya shule yetu" alisema.

Awali Naibu Waziri alitoa agizo hilo mwezi Novemba, 2016 alipofanya ziara ndogo ya kutembelea Kata ya Chang’ombe ambapo alitoa agizo kwa halmashauri ya Manispaa Dodoma kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa matundu 20 ya vyoo, vyumba 8 vya madarasa pamoja na ukarabati wa vyumba viwili vya madarasa ifikapo tarehe 10 Januari, 2017 kabla ya msimu wa masomo kuanza.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.