Serikali yazindua mwongozo wa barabara za Vijijini

Na.Mathew Kwembe

Serikali yazindua mwongozo wa barabara za Vijijini

Serikali imezindua mwongozo wa mpango na usanifu wa ujenzi wa barabara zinazopitisha magari machache kwa lengo la kutoa maelekezo na kuwawezesha wahandisi wanaofanya usanifu wa barabara hizo kutumia gharama nafuu za ujenzi.

Akizindua kitabu cha mwongozo huo tarehe 3 Februari, 2017 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema kuwa mwongozo huu utaiwezesha Serikali kujenga barabara nyingi na gharama nafuu.

"Ujenzi na ukarabati wa barabara zinazopitisha magari chini ya 300 kwa siku utakuwa wa gharama nafuu, hivyo mwongozo huu utasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili barabara nyingi hususan za vijijini," amesema Katibu Mkuu.

Amewataka wahandisi na Mafundi ujenzi kutumia mwongozo huo katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuweza kusaidia kazi na miradi mbalimbali ya barabara kuweza kufanyika kwa viwango vilivyo bora na gharama nafuu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Miundombinu kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Dokta Fikiri Magafu alisema kuwa Ofisi yake kama mtumiaji mkuu wa mradi huo watafaidika sana na kuwepo kwa mwongozo huo ambao unalenga kusaidia ujenzi wa barabara hizo kwa gharama nafuu.

Aliongeza kuwa kupitia mwongozo huo, barabara za vijijini zitajengwa kwa nusu ya gharama kulinganisha na gharama zinazotumika hivi sasa.

Kwa mujibu wa Meneja wa huduma za Kiufundi kutoka taasisi inayojishughulisha na Utafiti ya AFCAP bwana Nkululeko Leta, mwongozo huo umeandaliwa na taasisi yake kufuatia maombi kutoka TAMISEMI, na unatokana na uzoefu uliopatikana kutoka nchi kadhaa za Afrika ambazo pia zilitekeleza mwongozo kama huo.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.