Serikali yataka wanasheria wasimamie vyema kesi za Halmashauri

Na.Shani Amanzi na Mwajuma Ally

Serikali yataka wanasheria wasimamie vyema kesi za Halmashauri

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mhe.Selemani Jafo, Jafo amewataka wanasheria katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha kuwa wanasimamia vyema kesi zinazohusu halmashauri hizo ili kuepuka kuisababishia hasara serikali ambayo inatokana na kutotekeleza vizuri majukumu yao.

Akifungua mafunzo ya siku tatu ya wanasheria wa halmashauri zote nchini mkoani humo jana, Mhe.Jafo alisema zipo kesi nyingi zinazohusu halmashauri mbalimbali, lakini zinashindwa kutetewa na kusababisha serikali kulipa fidia.

"Licha ya kuwapo wanasheria ndani ya halmashauri hizo, lakini wanashindwa kusimamia kesi zinazowakabili hali inayochangia serikali kulipa gharama kubwa kwa washindi wakati fedha hizo zingetumika kwa maendeleo ya wananchi," alisema Jafo.

Alisema fedha zinazolipwa na serikali mara baada ya kushindwa kesi, zingeweza kusaidia maendeleo ya wananchi ndani ya halmashauri hizo kutokana na wanasheria kutokuwa makini.

Aidha, Naibu Waziri aliwataka wanasheria hao kuhakikisha wanasimamia vyema kesi za ardhi zinazowakabili wananchi wa chini ambao wengi wao hudhurumiwa na wenye uwezo na kusababisha malalamiko kwa wasimamizi wa sheria.

"Nawaomba wanasheria nyie kuhakikisha mnasimamia kesi za za ardhi ipasavyo ili wananchi wa kawaida wasio na haki waweze kupata haki zao kisheria," alisema.

Hata hivyo, Mhe.Jafo alisema sheria za halmashauri nyingi zinatofautiana na maeneo husika ma kuwa na matatizo makubwa ya kimaandishi kutokana na kukinzana na sheria mama.

Alisema kutokana na sheria hizo kutoeleweka, inasababisha mikataba mingi ndani ya halmashauri hizo kutokuwa na umakini kwa kutoipendelea serikali na kuwapa kipaumbele walioingia mikataba hiyo, hali inayoonyesha kama hawapo wanasheria.

"Toeni upendeleo kwa serikali pale mnapoingia mikataba, lakini wanasheria wengi mnashindwa kufanya hivyo hali inayosababisha serikali kushindwa kufanya lolote pale muingia mkataba anaposhindwa kutimiza wajibu wake wa kazi," alisisitiza Mhe.Jafo.

Pia alisema ipo migogoro mingi katika uendeshaji wa vikao vinavyosimamiwa na halmashauri, hali ambayo inatakiwa wanasheria hao kutenda haki.

Alisema kila mmoja anatakiwa kutimiza wajibu wake katika kutenda yale ambayo yanampasa eneo lake la kazi badala ya kulaumiana ama kulaumiwa kila wakati.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.