Waziri aitaka Tume ya Utumishi wa Walimu kufanya kazi kwa uadilifu

Na Sylvia Hyera

Waziri aitaka Tume ya Utumishi wa Walimu kufanya kazi kwa uadilifu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. George Simbachawene (Mb) ameitaka Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu ili kufanikisha ufanisi na kuepuka udanganyifu katika utendaji wake.

Mhe. Simbachawene aliyasema hayo katika kikao kazi cha chombo hicho kilichoambatana na kuapishwa kwa wajumbe wapya wawili katika ukumbi wa Nyaraka za Taifa Dodoma hapo jana ambapo aliwataka watendaji wa Tume hiyo kufanya kazi kwa uweledi mkubwa ili kufikia malengo ya Tume na kukidhi haja ya wananchi kwa ujumla.

Aliongeza kuwa matarajio ya chombo hiki ni kikubwa hivyo watendaji wanatakiwa kutekeleza majukumu yao yakiwemo kuendeleza na kusimamia utumishi wa walimu, kuajiri kupandisha vyeo na kuchukua hatua za kinidhamu kwa walimu na kumshauri waziri mwenye dhamana na Serikali za mitaa masuala mbalimbali yanahusiana na Tume hiyo.

"Katika sheria ya Mwaka 2015 kifungu namba 5 kimeainisha majukumu ya chombo hiki , matarajio ya Serikali na Wananchi ndio yaliyofanya kuanzishwa kwa chombo hiki na kimepewa dhamana kubwa kustawisha sekta ya elimu na kupaza sauti kwa niaba ya walimu," alibainisha Mhe.Simbachawene.

Aidha Mhe. Waziri alieleza kuwa Tume hii ni chombo cha haki ili kufanya kazi kwa umakini lazima watendaji wawe waadilifu kuanzia kwenye ngazi ya wilaya ambao watakaoenda sambamba na mabadiliko ya sekta ya elimu na kama hawatenda haki basi chombo hiki kitashindwa kutimiza majukumu yake ambayo yatafanywa na vyombo vingine rasmi au sio rasmi .

Pia aliwataka wajumbe na watendaji wote kuwa makini katika mada zote zinazowasilishwa katika kikao kazi hicho ili kuendeleza uweledi walinao utakaofanikisha utendaji kazi wa Tume hiyo na kuhakikisha kazi inafanyika bila udanganyifu na upendeleo wowote.

Kwa upande wake Costantine Mashoko ambaye ni mjumbe wa Tume hiyo amehaidi kuwa wajumbe watashirikiana na sekretarieti, Mwenyekiti, Katibu wa Tume pamoja na wadau mbalimbali wa elimu ili kutekeleza majukumu kwa uweledi na kuhaidi kuteua watendaji waaminifu ngazi ya wilaya watakaotenda kazi kwa haki.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.