Serikali kuendelea kutatua changamoto sekta ya afya

Na.Fred Kibano

Serikali kuendelea kutatua changamoto sekta ya afya

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Selemani Said Jafo, amefanya ziara katika Halmashauri Manyoni na halmashauri mpya ya ambapo amebaini uwepo wa changamoto mbalimbali ikiwemo dawa katika Kituo cha Afya Itigi na Hospitali ya wilaya ya Manyoni mkoani Singida.

Akizungumza katika ziara hiyo, Mhe.Jafo amesema baada ya kutembelea Halmashauri hizo amebaini changamoto za dawa katika kituo cha afya Itigi pamoja na vifaa katika chumba cha kujifungulia akina mama huku akisema zipo changamoto ambazo zinazotakiwa kutatuliwa ndani ya halmashauri hiyo.

Mhe.Jafo amezungumzia kuhusu suala la upatikanaji wa dawa, kuwa tatizo hilo linaonekana ni kikwazo kutokana na watendaji kushindwa kutumia fedha za dharura wanazopewa na Serikali kununulia dawa na vifaa tiba.

“Naziagiza Halmashauri hizi kuhakikisha zinaweka kipaumbele uboreshaji wa vituo vya Afya kwa kununua dawa nyingi na vifaa vingine tofauti nakusubiri dawa zinazotoka Bohari ya Madawa (MSD)”, alisisitiza Naibu Waziri.

Aidha, amewaagiza watendaji wa Idara mbalimbali kuhakikisha wanashirikiana na Mkurugenzi wa Itigi ili kutimiza wajibu wao na kuifanya halmashauri hiyo kuwa bora na kuwaonya kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Katika hatua nyingine amewaasa watumishi wa halmashauri za Itigi na Manyoni kufanya kazi kwa bidii, weredi, ubunifu na sheria katika kuwahudumia Watanzania wote bila ubaguzi kwani wanamatarajio makubwa kutoka Serikali ya awamu ya tano.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.