Watendaji waagizwa kutekeleza agizo kuhusu wafanyabiashara

Na.Fred Kibano

Watendaji waagizwa kutekeleza agizo kuhusu wafanyabiashara

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George B. Simbachawene (Mb) amewataka Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Mamlaka zote za Serikali za Mitaa nchini wajipange kutekeleza usimamizi wa agizo la Mheshimiwa Rais la kuwaondoa Wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu Wamachinga kwa ufasaha, weledi na umakini mkubwa ili kusaidia kufanya biashara zao za kujipatia kipato na Mamlaka zote ziwachukulie wamachinga kama fursa na siyo changamoto.

Mhe. Simbachawene ametoa rai hiyo mjini Dodoma leo wakati akiongea na Waandishi wa habari ofisini kwake juu ya ukiukwaji wa agizo la Mhe. Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli la tarehe 6 Desemba, 2016 kuhusu zoezi la kusitisha uhamishaji wa Wafanyabiashara ndogondogo maarufu wamachinga.

Mhe. Simbachawene aliongeza kuwa maagizo ya Mheshimiwa Rais yanaonesha ambavyo anawependa na kuwathamini wamachinga hivyo, wasiondolewe kwenye maeneo yao kwa sasa hadi watakapotengewa maeneo mbadala, utaratibu wa kuwapangia maeneo uzingatie ushirikishwaji, pale inapowezekana wanaweza kupangiwa maeneo katikati ya mji na pia wawekewe utaratibu wa kupangiwa maeneo ya shughuli zao yenye miundombinu rafiki, wateja wa kutosha na pia washirikishwe wakati wa maandalizi ya maeneo hayo.

Aidha Mhe. Simbachawene amewataka Wafanyabiashara hao kutafsiri agizo la Mheshimiwa Rais kama fursa kwao na kwamba Mhe. Rais anawathamini na kuheshimu mchango wao katika uchumi wa Taifa lakini pia Mhe. Rais hakumaanisha kuwa wafanye biashara zao mahali popote kiholela bila kuzingatia sheria zilizopo bali watambue haki za watu wengine katika kufanya shughuli zao.

Kwa upande mwingine Mhe. Simbachawene amewaagiza Makatibu Tawala wa Mikoa ya Rukwa na Arusha ambako kuna shule za bweni za Makuyuni (Arusha) na Milundikwa (Rukwa) wanawatafutia shule wanafunzi waliopo katika shule hizo kwa sasa ndani ya mikoa walipotoka wakishirikianna na Makatibu Tawala wa mikoa husika ili wapangiwe shule mapema na wajue shule watakazo pelekwa kabla ya muhula mpya mwezi, januari, 2017 pia zoezi hili kutowavuruga wanafunzi wa kidato cha sita ambao tayari wamesajiliwa kwa ajili ya kufanya mtihani wa Taifa mwaka ujao.

Aidha, amewaagiza Makatibu Tawala wa Mikoa hiyo kuhakikisha kuwa walimu na watumishi wasio walimu ambao walikuwa wanafundisha katika shule hizo wanapangiwa shule zitakazopokea wanafunzi hao ili kutoathiri mwendelezo wa mada walizokuwa wakifundisha.

Awali majengo ya shule hizo yalikuwa makambi ya Jeshi la kujenga Taifa (JKT) na baadae Halmashauri zilipatiwa kuyatumia majengo hayo kama shule za sekondari za bweni lakini kutokana na kuongezeka kwa shughuli za Jeshi, Serikali imelazimika kuwahamishia wanafunzi katika shule nyingine zilizopo katika mikoa waliyotoka.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.