Naibu Waziri ataka wakandarasi wazembe wasipewe kazi Dodoma

Na.Shani Amanzi na Sylvia Hyera

Naibu Waziri ataka wakandarasi wazembe wasipewe kazi Dodoma

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Suleimani Jafo amewaagiza Wahandisi wa Mradi wa maji na Ujenzi uliopo katika shule ya sekondari Manzase, wilayani Chamwino kukamilisha mradi huo na kuacha kupeana kazi kwa mazoea.

Mhe. Selemani Jafo amefanya ukaguzi wa miradi ya maji na ujenzi katika kata ya Manzase wilayani Chamwino, mkoani Dodoma ambapo hakuridhishwa na kasi ya ujenzi wake licha ya kufikia Zaidi ya asilimia 70.

Aidha, Mhe. Jafo ametoa muda wa wiki mbili kwa mkandarasi wa ujenzi wa majengo Bwana S.A.Kalli wa kampuni ya Shamoka Building and Civil Building contractors Ltd kukamilisha kazi hiyo. Mhe.Jafo anatarajia kufungua mradi huo wa ujenzi na kisima cha maji mapema mwezi january, 2017.

Ujenzi huo wa nyumba sita zilizounganishwa kwa pamoja(six in one) kwa ajili ya kuishi walimu wa sekondari na madarasa mawili ni baadhi ya miradi inayofadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia Mradi wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu ya Sekondari (SEDP) na pia mradi wa tanki la maji ambayo yote ipo kijijini Manzase.

Mhe. Jafo amesema kumekuwa na uchelewaji wa ujenzi kutokana na kukosekana kwa mafundi katika eneo la ujenzi kwa wakati na kusema kuwa "kama leo wanakamilisha matatizo madogo madogo ya kiufundi na bado hayajakamilika inaonesha wazi mhandisi wa ujenzi wa shule aliyokabidhiwa kujenga hana uongozi mzuri kwani majengo yangekuwa yameshakamilika, na inawezekana kazi mmegawana kirafiki, haiwezekani apewe kazi zote za ujenzi katika maeneo tofauti pasipo kukamilisha ujenzi mmojawapo kwa wakati."

Vilevile, Naibu Waziri hakufurahishwa na ubora wa majengo ya nyumba za walimu kutokana na kuwa na dosari za kuta kupinda na kumtaka Mkurugenzi kuhakikisha majengo hayo yanakamilika hadi ifikapo mwishoni mwa mwezi desemba na kama hayajakamilika mkandarasi huyo asipewe kazi za ujenzi mkoani Dodoma, "kama hayajakamilika ni marufuku mhandisi wa ujenzi wa shule hii kupewa kazi ya serikali popote katika halmashauri za mkoa wa Dodoma," amesisitiza Mhe.Jafo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino Bw. Athuman Masasi amesema alikwishatoa maagizo na ameshafanya ziara sehemu hiyo na kuwataka wakandarasi hao kumaliza mradi katikati ya mwezi desemba mwaka huu.

Naye Diwani wa kata ya Manzase Mheshimiwa Peter Madanya amelalamikia hali mbaya ya huduma ya maji na kwamba wananchi wanatembea umbali mrefu kutafuta maji, “hali ni ngumu ya maji, wananchi wanatembea kilomita nyingi kufuata maji, wengine wanahatarisha maisha barabarani kwa ajili ya ajali, naomba Mheshimiwa Naibu Waziri utusaidie mradi huu uishe”

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.