Serikali yataka siku ya walemavu iadhimishwe mikoani

Na.Shani Amanzi


Serikali yataka siku ya walemavu iadhimishwe mikoani

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa amewaagiza Wakuu wa Mikoa kuhakikisha kuwa wanafanikisha maadhimisho ya siku ya walemavu Duniani kitaifa, katika mikoa yao badala ya walemavu kukusanyika jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa, Mhe. Waziri wa Nchi amesema kufanya hivyo kutasaidia kupunguza gharama badala ya walemavu wa vyama mbalimbali kusafirishwa jijini Dar es salaam kwa ajili ya kushiriki maadhimisho hayo.

AKauli ya Mheshimiwa Simbachawene inafuatia ombi la Chama Cha Walemavu kuomba Serikali kupitia halmashauri za wilaya kuwasafirisha wanachama wa vyama vya walemavu ili wafanye maadhimisho hayo kitaifa jijini Dar es salaam siku ya tarehe Desemba 3, 2016

" Kwa hiyo nichukue nafasi hii kuwaagiza Wakuu wa Mikoa na halmashauri kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha kwa vyama vya walemavu ili viweze kufanikisha maadhimisho hayo," amesisitiza Mhe.Simbachawene.

Mhe.Simbachawene amesema, kufuatia maelekezo hayo ya serikali sasa shughuli hizo zifanyike maeneo ya mikoa yao na wilaya zao.

Aidha, Mhe. Simbachawene ametoa pongezi kwa vyama vyote vya walemavu nchini kwa namna wanavyoshirikiana na kutoa maoni yao kwa Serikali, lakini pia Serikali ipo pamoja nao na wataendelea kushirikiana nao kuweka mbele maslahi yao, kutatua matatizo yao na katika hili shughuli ya kuadhimisha siku ya walemavu duniani Serikali ipo pamoja nao.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.