Waziri Simbachawene ataka watumishi wajitathmini utendaji wao wa kazi

Na.Fred Kibano

Waziri Simbachawene ataka watumishi wajitathmini utendaji wao wa kazi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene amewataka watumishi wa umma katika Ofisi yake watumishi kujitathmini iwapo huduma wanazotoa kwa wananchi zinakidhi matarajio ya Watanzania.

Mhe. Simbachawene ameyasema hayo wakati akitoa hotuba ya ufunguzi wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kilichofanyika mjini Dodoma.

Alisema ni vema watumishi wa umma wakafanya kazi kwa kufuata kanuni na taratibu za utumishi ili kuongeza tija mahali pa kazi.

"Kila mmoja anapaswa kutafakari haki zake na zile anazopewa je zina usawa, kwani watumishi wengi wanadhani ni marupurupu ama kuongezewa mshahara kwani ni zaidi ya hayo ikiwemo namna anavyochukuliwa na namna anavyo adhibiwa pale anapokosea na kupewa pongezi pale wanapofanya vizuri," amesema Mhe. Simbachawene.

Pia Mhe. Simbachawene amesema Wakuu wa kila Idara na Vitengo na watumishi wanapaswa kutatua tatizo la ubinafsi kwani mfanyakazi anapofanya vizuri ni yeye ndiye anayepaswa kupewa pongezi na siyo bosi wake kujiongezea mshahara.

"Sisi Viongozi tunapaswa kutafakari mwisho wa siku tunafanya vizuri ama tunaumizana," amesisitiza Mhe. Simbachawene.

Vilevile, Mhe. Simbachawene amesema kuna umuhimu wa kujua kila shilingi inayotumikaje na lazima ionyeshe matokeo yake ni nini na kila robo mwaka ya Utekelezaji wa Bajeti kwani kwa kufanya hivyo itawasaidia sana na kuongeza ufanisi wa kazi.

"ifike wakati tunafanya yanayopaswa kufanywa,sisi ni watumishi wazuri ila tatizo linakuja kwenye utekelezaji kwani dhana ya uwajibikaji wa Umma, nidhamu ya Utumishi wa Umma inapaswa iendelee kuimarika," amesema.

Ameonya kuwepo kwa hali ya rushwa hasa kutoka kwa walimu wanaohitaji kuhamia sehemu nyingine kwani kuna watu wameanzisha vijiwe mitaani na kutumia tovuti zisizo rasmi kwa kutapeli fedha za walimu wanaohitaji huduma hiyo, hivyo basi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inaendelea na uchunguzi na kwa wale watakaobainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Mhe. Simbachawene alihitimisha kwa kusema " Kauli ya hapa kazi tu inapaswa kutekelezwa na watumishi ili kufuata taratibu na kanuni za kikazi na jukumu la kusimamia Serikali za mitaa na Halmashauri ni letu sote kwani suala la maadili ni muhimu ili kuepuka vitendo vya rushwa."

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.