Waziri ataka Bodi Chuo cha Serikali za Mitaa kushughulikia malalamiko

Na. Sylvia Hyera

Waziri ataka Bodi Chuo cha Serikali za Mitaa kushughulikia malalamiko

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), Mhe.George Simbachawene, ameiagiza bodi ya chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo mkoani Dodoma (LGTI), kuyafanyia kazi malalamiko ya vitendo vya rushwa ya ngono katika idara ya taaluma na mitihani.

Mhe.Simbachawene ametoa agizo hilo tarehe 25 Novemba, 2016, wakati alipokuwa akizungumza na wanafunzi pamoja na uongozi wa chuo hicho wakati wa mahafali ya nane ya chuo hicho.

Amesema katika moja ya maeneo ambayo hajaridhishwa nayo, idara ya mitihani ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wanafunzi juu ya urasimu uliopo hasa wakati wa wanafunzi wanapo hitaji matokeo yao.

Aidha, Waziri Simbachawene amesema malalamiko mengi yamekuwa katika idara hiyo kwa kipindi kirefu lakini uongozo wa chuo hicho umeendelea kulikalia kimya bila kuchukua hatua.

"Naiagiza bodi ya chuo kuhakikisha kuwa idara hii inachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kuifumua na kuiunda upya kwani malalamiko haya yamekuwa ya muda mrefu watu wanaohusika na idara hii wamekuwa na ukilitimba wa hali ya juu mwanafunzi anapotaka kupata matokeo ya mitihani yake ni atazungushwa kama nini," amesema Mhe.Simbachawene.

Amesema hali hiyo imekuwa ikiashiria uwepo wa vitendo vya rushwa mbaya ya ngono kati ya wahusika wa idara ya mitihani na wanafunzi wa kike lakini pia wanafunzi wa kiume kudaiwa fedha.

"Naomba mlifanyie kazi suala hili haraka sana kwani haya malalamiko mimi ninayo kwa mda mrefu lakini na shangaa uongozi mmekaa kimya hali ambayo imefikia hatua hata kama mwanafunzi kalipia ada ya hosteli lakini bado atazungushwa hadi muhusika mwentee apende utazani anaomba bure,"amesema.

Aidha aliongeza kuwa kitu kingine ambacho anautaka uongozi wa chuo hicho kukifanyia kazi ni namna ya matumizi ya fedha za chuo kwani kumekuwepo na upotevu wa fedha lakini hakuna hatua zilizochukuliwa kwa waliohusika.

"Fedha za chuo zimeibiwa na wahusika wapo hadi hii leo lakini hakuna kilichuuliwa naomba wahusika wasimamishwe haraka ili uchuguzi ufanyike na hatua zingine kuchukuliwa kwa wahusika," alisema.

Hata hivyo amesema kuwa kuna kila sababu ya serikali kutengeneza utaratibu ambao utakuwa unatumika katika kuwaajili wanafunzi wanaomaliza katika chuo hicho ambao wanataaluma ya utumishi katika mamlaka za serikali a mitaa.

"Serikali inatumia takribani bilioni 8.3 kwajili ya kuendesa chuo hichi kilamwaka lakini wanafunzi wanapotoka hapa wanakosa kazi hali ambayo si sahihi kutokana na uwezkezaji huo unaofanywa na serikali kwa mwaka kwani hata ujenzi wa chuo hiki umeghalimu sh. bilioni 36.5 hivyo ni lazimu wahitimu hawa tuwatumie ipasavyo,"alisema

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya chuo hicho Prof. Suleiman Ngware alisema kuwa maagizo yote yaliyotolewa na Waziri atayafanyika kazi haraka iwezekanvyo na wahusika wote watachukuliwa hatua.

"Mheshimiwa Waziri yote uliyoagiza tutayafanyia kazi na hatua kali zitachuliwa kwa wahusika wote bila ya kumuonea mtu," amesema Prof. Ngware.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.