Naibu Waziri akerwa na kasi ndogo ujenzi madarasa Sekondari ya Kibuta

Na. Mathew Kwembe

Naibu Waziri akerwa na kasi ndogo ujenzi madarasa Sekondari ya Kibuta

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amekerwa na kasi ndogo ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa, nyumba ya walimu yenye uwezo wa kutumiwa na walimu sita pamoja na ujenzi wa vyoo katika Shule ya Sekondari ya Kibuta iliyopo kata ya Kibuta wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani.

Mhe.Jafo alionyesha kukerwa zaidi na kasi ya ujenzi wa mradi huo, mara baada ya kufika shuleni hapo na kukuta mafundi wachache wakiendelea na ujenzi wa nyumba itakayotumiwa na walimu 6, ambapo ujenzi wake umefikia madirishani, na katika ujenzi wa madarasa matatu na vyoo kukiwa hakuna shughuli yoyote ya ujenzi inayoendelea.

Akizungumza mbele ya wajumbe wa kamati ya fedha na wakuu wa Idara wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Mhe.Jafo alimpa mkandarasi huyo siku 45 awe amemaliza shughuli zote za ujenzi wa mradi huo na kuahidi kuitembelea tena shule hiyo tarehe 15 desemba, 2016.

"Mkurugenzi, itakapofika tarehe 15 desemba, 2015 nitakuja tena katika shule hii na nataka nikute mkandarasi yupo katika hatua za mwisho mwisho za kukamilisha mradi huu," alisema Mhe Naibu Waziri na kuongeza: "haiwezekani fedha hizi tupewe siku moja na wenzetu wa shule nyingine nchini zinazotekeleza mpango huu wa kuboresha elimu ya sekondari ilhali wenzetu wamekamilisha ujenzi wa majengo yao tena kwa kutumia mafundi wa ndani wakati sisi tunaendelea kusua sua, haiwezekani," alisema Mhe.Jafo.

Aidha Naibu Waziri alimtaka Mkandarasi anayejenga mradi huo kuhakikisha anakamilisha ujenzi huo mapema iwezekanavyo kwani hakutakuwa na muda wa nyongeza pindi muda uliowekwa kukamilisha mradi huo utakapofika na kumtaka msaidizi wa mkandarasi huyo kumpa taarifa mkandarasi juu ya uamuzi huo wa serikali.

"Hakuna excuse ya aina yoyote kazi iwe imekamilika. Hatuzidi siku 45 mpaka sasa, naangalia labour power ni ndogo sana hapa site. Kamwambie boss wako tunataka hii kazi tarehe 15 disemba tukute mnafanya final touches. Tumetoa fedha na tunataka fedha itumike kama ilivyokusudiwa," alisisitiza Naibu Waziri.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri, fedha za mradi wa ujenzi wa madarasa matatu, nyumba yenye uwezo wa kutumiwa na walimu sita na vyoo katika Shule ya Sekondari ya Kibuta zilitolewa na Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kati ya mwezi juni na Julai mwaka huu, na kwamba baadhi ya shule zinazotekeleza miradi ya aina hiyo zimekwishakamilisha ujenzi wake.

Aliongeza kuwa hivi karibuni alitembelea baadhi ya shule zinazotekeleza miradi ya aina hiyo katika wilaya za Bariadi na Igunga na kukuta ujenzi wa miradi ya aina hiyo ikitekelezwa kwa kasi kubwa na ubora wa hali ya juu tofauti na hali aliyoiona katika Shule ya Sekondari ya Kibuta.

Hivyo, Mheshimiwa Jafo akamtaka Mhandisi wa ujenzi wa wilaya ya Kisarawe Godfrey Mbena kuhakikisha kuwa anasimamia kikamilifu mradi huo wa ujenzi ili ukamilike kabla ya tarehe 30 desemba 2016.

Mapema Mhandisi Mbena alimweleza Naibu Waziri kuwa shule ya Sekondari Kibuta ni miongoni mwa shule 528 ambazo zinatekeleza mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa, ujenzi wa nyumba ya walimu, ujenzi wa matundu ya vyoo na tanki la maji lenye ujazo wa lita elfu thelathini.

Aliongeza kuwa hadi kufikia sasa asilimia 50 ya ujenzi imekamilika ambapo kazi iliyobaki inatarajiwa kukamilika katika kipindi cha mwezi mmoja na nusu kilichosalia.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.