Serikali yataka walimu nchini wajitume kufundisha Shule za Sekondari

Na. Mathew Kwembe

Serikali yataka walimu nchini wajitume kufundisha Shule za Sekondari

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amewataka walimu nchini kuongeza bidii katika ufundishaji wa masomo ili kuwawezesha wanafunzi wanaosoma katika shule hizo wafaulu kwa kiwango cha hali ya juu.

Akizungumza na walimu wa shule ya sekondari ya kata ya Chanzige iliyopo wilayani Kisarawe jana, Naibu Waziri alisema kuwa miaka ya nyuma shule za sekondari za serikali zilikuwa na walimu wachache lakini kutokana na kuzingatia suala la ufundishaji waliweza kutoa idadi kubwa ya waliofaulu kulingana na hali ilivyo hivi sasa.

Naibu Waziri aliongeza kuwa kipindi anasoma hali ya ufaulu ilikuwa kubwa kutokana na kuwepo kwa hamasa kubwa ya ufundishaji na ujifunzaji kutoka kwa walimu na wanafunzi, huku akitolea mfano wa shule za sekondari za kata kushindwa kufanya vizuri hata masomo yasiyo ya sayansi.

Alisema kuwa ingawa kwa muda mrefu sasa kilio cha baadhi ya shule za sekondari za kata kimekuwa ni kukosekana kwa maabara hasa kwa shule ambazo zimekuwa zikipokea wanafunzi wa sayansi, lakini Mheshimiwa Jafo ameeleza kuwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne kimekuwa duni hata kwa baadhi ya masomo yasiyo hitaji maabara

Naibu Waziri alieleza kushangazwa kwake na ufaulu duni katika masomo licha ya ukweli kwamba wanafunzi wamekuwa wakifeli hata masomo yasiyojitaji matumizi ya maabara.

Aidha Mhe.Jafo aliongeza kuwa pamoja na shule za kata kukosa idadi kubwa ya walimu lakini hali ya ufundishaji imekuwa duni ambapo wanafunzi wamekuwa wakifeli hata masomo ya sanaa.

"Kama shida ni maabara, iweje wanafunzi wetu wafeli somo la Kiswahili au masomo mengine yasiyo ya sayansi," alisema.

Aliongeza kuwa baadhi ya shule zina walimu wa kutosha wa masomo ya sayansi na sanaa lakini bado kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi kipo chini, na hivyo amewasihi walimu kujituma kwa bidii ili kuwafundisha watoto ili waweze kuelewa walichojifunza lakini pia kufaulu vizuri masomo yao.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri alielezwa na baadhi ya walimu wanaofundisha shule ya sekondari ya kata ya Chanzige kuwa changamoto kubwa zinazoikabili shule hiyo ni pamoja na ukosefu wa hosteli ambayo ingetumika na wanafunzi hasa wa kike ili waweze kujiepusha na makundi yasiyo mazuri kwa wanafunzi hao.

Mmoja wa walimu hao Lucy Mhilu alimweleza Naibu Waziri kuwa tatizo kubwa linaloshusha ufaulu wa wanafunzi katika shule ya Sekondari Nyanzige ni kukosekana kwa mazingira bora ya kujifunzia wanafunzi hao hasa baada ya kutoka darasani na hivyo kumuomba Mhe.Jafo uwezekanao wa kuwatafutia hosteli wanafunzi hao ili waweze kusoma vizuri.

Wakati huo huo kampuni inayotoa huduma ya usafirishaji wa anga Qatar Airways nchini Tanzania imechangia madawati 100 katika shule ya msingi Chanzige B, iliyopo wilayani Kisarawe, mkoani Pwani, ikiwa ni sehemu ya mradi wa kusaidia juhudi za serikali kupitia mpango wa kuondoa uhaba wa madawati nchini kwa shule za msingi pamoja na sekondari hii ni pamoja na sehemu ya kurudisha shukrani kwa jamii.

Madawati hayo yalipokelewa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe.Selemani Jafo katika shule ya Nyanzige B wilayani Kisarawe.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.