Manispaa ya Dodoma waagizwa kukagua changamoto zilizopo shuleni

Na. Fred Kibano

Manispaa ya Dodoma waagizwa kukagua changamoto zilizopo shuleni

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewataka viongozi wa Manispaa ya Dodoma kufanya ukaguzi wa shule ili wajue changamoto zinazowakabili walimu na wanafunzi.

Akizungumza na Afisa Elimu wa Manispaa ya Dodoma Bi. Scola Kapinga pamoja na watendaji wengine wa Manispaa hiyo baada ya kufanya ziara fupi ya kuitembelea shule ya msingi Chadulu kubaini changamoto zilizopo katika shule hiyo Mhe. Jafo alisema shule hiyo ni mojawapo ya shule zilizopo kati kati ya mji lakini mazingira yake hayaridhishi.

Mhe. Jafo alisisitiza kuwa mazingira ya vyoo vya shule yanatakiwa kuwa rafiki ili kuepukana na mlipuko wa magonjwa kama kipindupindu ambayo yamekwishaanza kuripotiwa katika baadhi ya maeneo.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chadulu Bwana Kassian Henry alimwambia Naibu Waziri kuwa miongoni mwa changamoto zinazowakabili shuleni hapo kuwa ni miundo mbinu mibovu ya vyoo tangu alipohamia katika shule hiyo mwaka 2009.

"Ifikapo Jumatano ijayo tarehe 16 November, 2016 muwe mmemaliza kutengeneza miundo mbinu katika vyoo vya walimu pia changamoto ya maji itatuliwe kwavile gharama zake ni laki sita kwa mujibu wa Mhandisi .Nitakuja kuangalia utekelezaji wa agizo hili," alisema Mhe. Naibu Waziri.

Mmoja wa walimu wa shule hiyo Jacqueline Chaula amesema changamoto ya choo kwao imekuwa kero kwa muda mrefu na wakitaka kujisaidia inawalazimu kwenda kuomba nyumba za jirani au muda mwingine inawalazimu kumwaga maji mengi na kusubiri kwa muda kitu ambacho kinawatesa sana endapo mtu anakuwa kabanwa na haja, pia hali hiyo imewaathiri kiutendaji kwavile wamekuwa wakikumbwa na magonjwa kama U.T.I.

Katika ziara hiyo Mhe Naibu Waziri alitembelea vyoo vya walimu pamoja na wanafunzi ambao kwa sasa wanatumia vyoo vya shimo vyenye matundu 10 kwa wasichana na matundu 10 wavulana, pia alitembelea jengo la mlinzi ambalo halijakamilika na kuutaka uongozi wa shule walikamilishe ili mlinzi na walimu wa mazoezi wanaokuja kwenye mafunzo wapate kujihifadhi.

Hii ni ziara yake ya tatu kuifanya katika shule za msingi zilizopo Manispaa ya Dodoma katika majuma ya hivi karibuni ambapo alitembelea pia shule za Msingi Chang’ombe na Nzuguni.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.